Tuesday, March 20, 2012
Lowassa Atembelea Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro
| Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro. |
| Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu Mstaafu. |
| Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro. |
Neno La Leo: Wiki Ya Maji Na Helikopta Arumeru!
Ndugu zangu,
Nchi yetu inaingia gharama zisizo za lazima kama ambazo nchi inaingia kwa sasa kwa wagombea, vyama na hata Serikali kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo. Tumeona hata helikopta zenye gharama nyingi zikiruka kilomita nyingi angani eti kwenye harakati za kusaka kura kwenye chaguzi ndogo huku wananchi wengi wa jimbo husika wakitembea kilomita nyingi kusaka maji ya kunywa na kupikia.
Wiki kama hii ya Maji inayoendelea sasa ilipaswa kuwa wiki ya kuomboleza uhaba wa maji unaochangiwa pia na matumizi mabaya ya rasilimali za wananchi kama haya ya kuendesha chaguzi ndogo kule Arumeru Mashariki. Na hili ni Neno La Leo.
Monday, March 19, 2012
KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUJENGA MRADI WA UVUNAJI MAJI HOSPITALI YA WILAYA IRINGA
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)Teddy Mapunda kulia akisalimiana na Galus Lugenge Diwani wa kata ya Mwangata Frelimo, wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa uvunaji maji hospitalini hapo, anayefuatia ni Nandi Mwiyombela Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji (SBL), Caroli Lunyili Injinia wa maji Manispaa ya Iringa na kushoto ni Stella Kiwele Mganga mkuu msaidizi wa Hospitali ya Wilaya Iringa. Mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 20 na unatarajiwa kusaidia watu zaidi ya 150.000 katika manispaa hiyo wanaozunguka eneo la Hospitali.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili hospitalini hapo tayari kwa ukaguzi wa mradi wa Uvunaji maji unaojengwa katika hospitali hiyo, kulia ni Mwenyeji wake Stella Kiwele Mganga Mkuu msaidizi wa Hospitali ya Wilaya Iringa, na kushoto ni Nandi Mwiyombela Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji.Maalimu seif Akutana Na Wafanyakazi Wa Wizara
Waziri Chikawe Aongea Na Waandishi Wa Habari
Mama Salma Kikwete Mgeni Rasmi Maadhimisho Ya Maulidi Ya Wanawake Wa Kiislamu
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akiongea na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) kwenye sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad( SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro,(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kiwete akisalimiana na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania ( JUWAKITA) Mkoani Morogoro Machi 18.2012 alipohudhuria Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW). yalioandaliwa na jumiya hiyo ya JUWAKITA. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (vazi jeupe) akisindikizwa na Mwenyekiti Taifa wa (JUWAKITA) Shamim Khan, (kushoto) ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Halima Dendegu (wapili kutoka kulia) na Katibu Tawala Mkoa Morogoro Mgeni Baruwani baada ya kumaliza sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mke wa Rias na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete(kulia) na Mwenyekiti Taifa wa JUWAKITA Mama Shamim Khan kwa pamoja wakifuatilia ratiba katika Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) katika Chuo cha Kiislam- Morogoro.Maadhimisho hao yameandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) mkoa Morogoro,Machi 18 2012, (picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Wanajumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) mkoani Morogoro wakimkaribisha mgeni rasmi Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete hayupo pichani alipowasili kwenye maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Machi 18.2012. ( Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Akina mama mbalimbali wakimsikiliza mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akiongea na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) kwenye sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad( SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro,(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (vazi jeupe) akisindikizwa na Mwenyekiti Taifa wa (JUWAKITA) Shamim Khan, (kushoto) ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Halima Dendegu (wapili kutoka kulia) na Katibu Tawala Mkoa Morogoro Mgeni Baruwani baada ya kumaliza sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO). Sunday, March 18, 2012
Spika wa Bunge akutana na ujumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM)
Katibu Mtendaji wa APRM Bi. Rehema Twalibu akitambulisha
ujumbe wa wataalam wanaounda timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara
Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) kwa mhe.
Spika. Ujumbe huo ulifika Bungeni leo kukutana na uongozi wa Bunge kwa lengo la
kujadili maswala mbalimbali katika utawala bora
Mwenyekiti wa Bodi ya APRM Tanzania Prof Assa Mlawa akitoa
neno la utangulizi mara baada ya ujumbe huo kufika kuonana na Mhe Spika Ofisini
kwake leo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akijibu baadhi ya
maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala
ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) mara baada ya
ujumbe huo kukutana na uongozi wa Bunge dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni
kiongozi wa ujumbe huo Akere Tabeng Muna na kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya
APRM Tanzania Prof. Hassa Mlawa
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo mbele
ya wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika
(Africa Peer Review Mechanism –APRM) mara baada ya kukutana nao Ofisi za Bunge
Dar es salaam leo. Kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi ya APRM Tanzania Prof.
Hassa Mlawa na Mhe. Anne Makinda Spika wa Bunge na kushoto ni kaimu katibu wa
Bunge Charles Mloka. Ujumbe huo ulifika Bungeni leo kukutana na uongozi wa Bunge
kwa lengo la kujadili
Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa kamati za Bunge
wakisikiliza kwa makini baadhi ya hoja zilizokuwa zikiulizwa na baadhi ya
wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika
(Africa Peer Review Mechanism –APRM) ambao walikutana na uongozi wa Bunge leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya fedha za Umma (PAC) Mhe. John Cheyo
akijibu baadhi ya maswali kuhusu usimamizi wa Bunge katika maswala ya fedha za
umma kwa wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani
Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) ambao walikutana na uongozi wa Bunge
leo kujadili masala mbalimbali katika utawala bora
wajumbe wa timu ya
kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review
Mechanism –APRM) wakiwa katika kikao cha pamoja na Spika wa Bunge na wenyeviti
wa kamati za kudumu za Bunge mara baada ya kukutana nao Ofisi za Bunge Dar es
salaam leo. Saturday, March 17, 2012
Tendwa: Vincent Alikuwa Mtoto Mno Kujua Kifo Cha Mwl Nyerere
Tendwa alisema, ukweli wa kifo cha Mwalimu Nyerere, anayeufahamu
ni daktari wake katika hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyopo Uingereza, ambako
mwasisi huyo wa taifa, alilazwa na kupatiwa matibabu mpaka alipofariki
Alisema wakati Mwalimu Nyerere anafariki , Vincent alikuwa mtoto mdogo na kwamba taarifa hizo alipaswa kusema Chifu Wanzagi.
“Kwanza nashangaa sana, wakati Mwalimu Nyerere anafariki, Vincent alikuwa mtoto mdogo sana na kwamba hawezi kujua taarifa za kifo hicho labda awe amesimuliwa na baba yake Chifu Wanzagi ndiye mwenye jukumu la kuzungumzia kifo cha Mwalimu kwa sababu alikuwa kaka yake lakini, huyu ni kijana mdogo sana,” Tendwa alimshukia Vincent.

MY TAKE:
Kwa kauli kama hii
inayomshambulia Vincent tena Tendwa alitaka kufanya suluhu au ana lengo
lingine? kwani mwaka 1999 Vincent alikuwa mtoto kushindwa kujua kilichotokea
kwa baba yao ?.Nadhani
Tendwa amezidi sasa kufanya propaganda za CCM
Mdau Aliyekereka
Vicent Amlipua Tendwa, Mkapa Aomba Suluhu
Vicent Nyerere amemlipua Msajili wa Vyama vyaSiasa,
John Tendwa, kwa kumzuia kumzungumzia Hayati Mwalimu Nyerere.
Amemshauri kuwa kama anahitji kuwa mmoja wa familia
yao, anaruhusiwa kuandika barua kuomba kujiunga na ukoo wao kama alivyofanya
Mkapa.
Alisema anamshangaa Tendwa kumpiga marufuku kuongelea
mambo ya baba yake na kulidanganya Taifa kuwa watahatarisha amani nakujenga
chuki kwa Taifa kwa kumzungumzia Nyerere.
“Mimi huyu ni baba yangu na kila siku lazima nimtaje na
sisi wakatoliki tuna sala maalum ya kumwombea Nyerere na leo (jana) pia nimesali
mara baada ya kuamka, sasa yeye ni nani anayenizuia kutaja jina lababa yangu,
kama anataka ajiunge na ukoo wetu aombe kwa barua, kama alivyofanya mwenzake
Mkapa, aliandika barua akaingizwa katika ukoo,”alisema Nyerere.
Akimnadi Nassari katika mkutano wa hadhara wakampeni,
Vincent Nyerere, ambaye ni Meneja wa kampeni za mgombea ubunge waChadema Jimbo
la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, jana alisema kuwa Mkapa amemfuata Joseph
Butiku kuomba amuombea msamaha kwake (Vincent). Alisema kuwa Mkapa alimweleza
Butiku kuwa alikuwa anamtania ingawa mbunge huyo aliichukulia kauli ya Rais huyo
mstaafu kama ya kweli.
“Huyu Butiku jana (juzi) alinipigia simu akiniomba
tuachane na haya mambo ya malumbano kwa sababu Mkapa alikuwa ananitania na
hakujua kama itakuwa hivyo, na mimi nimeendelea kulisema hadharani, sasa anaomba
basi yaishe,”alisema Nyerere katika mkutano uliofanyika katikakijiji cha Msitu
wa Mbogo, Kata ya Mbuguni.
Alisema kuwa amekataa kuombwa radhi kupitia njia yasimu
au kukutana wawili na kuongeza kuwa anachotaka ni Mkapa kwenda Arumeru kuomba
radhi katika mkutano wa hadhara ambao aliuhutubia na kumchafua kuwa hanaundugu
na Hayati Mwalimu Nyerere.
Aidha, alisema Mkapa anapaswa kuwenda kumuomba radhi
kwenye ukoo wao. “Mimi ni wa ukoo wa Nyerere atake asitake, Nyerere ni baba
yangu na sitaacha kumtaja kamwe,” alisema Vincent.
Alisema kuwa Mkapa alikuwa anamheshimu sana kama Rais
mstaafu na alifahamu anahitaji kupumzika, ila kwa kumgusa kwa hilo nakumchafua
hadharani kuwa anajifanya mtoto wa Nyerere, wakati hamfahamu, kwa hilo aende
katika ukoo kumsafisha.
Mwakyembe Naye Arejea: Kutoa Neno Jumatatu
Na waandishi wetu
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amerejea nchini akitokea India alikokwenda kwa matibabu na kueleza kuwa atazungumzia, pamoja na mambo mengine, afya yake keshokutwa atakapoingia ofisini.
Hata hivyo, mara baada ya kuwasili jana alasiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam Mbunge huyo wa Kyela (CCM), hakutaka kuzungumza na waandishi wa habari na badala yake alitoa ujumbe wake huo kupitia kwa Mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa ambaye pia ni msemaji wa familia ya Dk Mwakyembe.
Mwambalaswa alisema Dk Mwakyembe aliona ni vyema apate muda wa kutosha kujiandaa kabla ya kukutana na waandishi wa habari Jumatatu.
“Afya yake imeimarika na anaendelea vizuri, ila ameomba msamaha kuwa hataweza kuzungumza na nyinyi (waandishi), amesema yeyote anayetaka kuzungumza naye, aende ofisini kwake Jumatatu,” alisema Mwambalaswa.
Dk Mwakyembe alifika katika viwanja hivyo saa 9:47 alasiri, lakini kabla ya kuingia katika vyumba vya abiria wanaowasili, alituma ujumbe kwa waandishi wa habari kuwa hatakuwa tayari kuzungumza jambo lolote.
Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo Oktoba 9, mwaka jana yalimlazimu kupelekwa katika Hospitali ya Appolo, India kwa matibabu zaidi.
Maradhi hayo yamezua utata mkubwa baada ya kudaiwa kuwa yametokana na kuwekewa sumu huku kukiwa na kauli mbalimbali zinazotofautiana kutoka kwake na baadhi ya watendaji wengine wa Serikali.
Kauli tata zaidi ziliibuka baada baadhi ya viongozi akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta kudai kuwa maradhi yanayomsumbua Dk Mwakyembe yametokana na kulishwa sumu.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba alijibu madai hayo aliposema kuwa uchunguzi wa polisi umebaini kuwa Dk Mwakyembe hajaugua kwa sababu ya kulishwa sumu na kutishia kuwachukulia hatua walitoa kauli hizo.
Ripoti ya uchunguzi aliyoisoma Manumba katika mkutano wake na waandishi wa habari Februari 16, mwaka huu Dar es Salaam, inaonyesha kuwa Dk Mwakyembe hakulishwa sumu huku akisema kwamba pia ulijumuisha taarifa kutoka hospitalini India ambako alikuwa anatibiwa.
Alisema uchunguzi huo unalipa Jeshi la Polisi picha kuwa waliotoa taarifa hizo hadharani wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Baada ya kauli hiyo, Dk Mwakyembe aliibuka na kutoa kauli nzito iliyoonekana kumjibu Kamishna Manumba akielezea kushangazwa kwake na majibu hayo huku akisisitiza kuwa madaktari waliokuwa wakimtibu walithibitisha kuwa ugonjwa alionao unatokana na kulishwa sumu.
Mbali ya Dk Mwakyembe, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, kwa nyakati tofauti walikana kuijua ripoti hiyo ya Kamishna Manumba.
Hata hivyo, katika kile kilichoonekana kudhamiria kuchukua hatua, inadaiwa kuwa Kamishna Manumba aliwasilisha jalada la mashtaka kwa watu hao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi ambaye alithibitisha kulipokea lakini akasema ni vigumu kufahamu ni lini atakapopeleka mahakamani jalada la kesi kwa watu hao.
Friday, March 16, 2012
Madaraka Nyerere Amuumbua Mkapa ( Gazeti Mwananchi)
ASEMA VINCENT NI MDOGO WAO, ATAKA TUHUMA ZINGINE AJIBU MWENYEWE
Waandishi wetu, Dar, Arumeru
MADARAKA Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ameibuka na kuthibitisha kuwa Mbunge wa sasa wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere ni mdogo wao na mwanafamilia hiyo, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, Josephat Kiboko Nyerere.
Kauli ya Madaraka imekuja siku chache baada ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, kudai kwamba hamtambui mbunge huyo kuwa ni miongoni mwa familia ya Mwalimu Nyerere kwani katika kipindi chote alichofanya kazi na Mwalimu, hakusikia jina hilo.
Jumatatu ya wiki, akizindua kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, Mkapa aliuambia umati uliohudhuria kwamba hakuwahi kusikia kama kulikuwa na mtoto wa familia hiyo aliyekuwa akiitwa Vincent Nyerere.
Kauli hiyo ilipingwa vikali juzi na Vincent akisema si jambo la ajabu Mkapa kutomfahamu yeye kwasababu Mkapa si sehemu ya ukoo wao huku akimrushia kombora kwamba akiwa madarakani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa Hospitali ya St Thomas, Uingereza, kinyume na matakwa ya familia yao na wakati huo huo, daktari wake Profesa David Mwakyusa alijua maradhi ya mwasisi huyo wa taifa.
Vincent alikwenda mbali zaidi na kumshambulia Mkapa kwa kuongoza ubinafsishaji holela enzi za utawala wake huku akimtuhumu kuuza viwanda na rasilimali za nchi kwa kisingizio cha ubinafasishaji.
Jana gazeti hili liliwasiliana na Madaraka kutaka kupata ukweli wa kauli hiyo ya Mkapa. Katika jibu lake fupi, Madaraka alithibitisha kuwa.... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com
Thursday, March 15, 2012
Hatimaye Rais Ateua Wakuu Mikoa Kwa Mikoa Mipya
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa.
Dkt. Rajab Mtumwa RUTENGWE ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.
Ndugu Magalula Saidi MAGALULA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.
Ndugu Paschal Kulwa MABITI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU. Kabla ya hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.
Kapt. Asery MSANGI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE. Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.
Uteuzi huu unaanza tarehe 15 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi.
Mwisho.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.15 Machi, 2012

Na Mzee Mkapa Ni Bingwa Wa Kukwepa Maswali!
( HII NI CHANGAMSHA BARZA!)
( Ndugu zangu wakati mwingine tunahitaji utani, tucheke na kutafakari. Hiki kisa ni cha kubuni. Kilipata kuletwa na mmoja wetu. Hakika kilichangamsha baraza haswa. Hapa nakirudia tu. Ni mambo ya kawaida tu, na katika enzi zake, Mzee wetu Mkapa alikuwa na staili yake ya kujibu na kutokujibu maswali! )

Rais Mkapa katika mapumziko yake ya kila Christmas alipokwenda nyumbani kwake huko Masasi, Mkoani Mtwara kwa ndege ya Serikali alizuru mojawapo ya Day Secondary Schools za hapo mjini na kutoa fursa kwa Wanafunzi kumwuliza maswali yo yote.
MKAPA: Nani atafungua dimba?
MASUMBUKO: Viongozi wa Serkali na wa Vyama vya Siasa wanatuambia kuwa Serkali ya Tanzania HAINA DINI. Lakini mbona ofisi zote za Serkali zinafungwa na Wafanyakazi wote Serkalini wanalazimika KUPUMZIKA KILA JUMAPILI?
MKAPA: Uliza swali lingine.
MASUMBUKO: Swali la nyongeza; Hivi ni kweli nayo JUMAMOSI ilipitishwa Bungeni iwe pia siku ya mapumziko minajili ya KUWAWEZESHA NA WASABATO wapumzike?
MKAPA: Mtoto mwingine?
CHAUSIKU: Katika Awamu ya Tatu kitabu maarufu kiitwacho "MWEMBECHAI Killings and the Political Future of Tanzania" kilipigwa marufuku kuuzwa na kuingizwa humu Nchini na hadi leo hakiruhusiwi kuonekana. Kisa? Tunanong'onezwa kuwa eti ni kwa sababu Kitabu hicho kinawakashifu mashabiki wazawa wa pale "MWEMBE-YANGA", Temeke - hiyo ni sahihi?
MKAPA: Na swali la lala-salama nani atauliza?
CHAUSIKU: Hapa nchini Makanisa yote yana Makao Makuu (Headquarters) nje ya Tanzania na yanaletewa misaada ya hali na mali miaka yote tokea Ukoloni na mda wo wote. Kulikoni misaada ya pesa inayoletwa kuboresha au kujenga Misikiti (ambayo maskini kuli hali mingi ni ya udongo na nyasi) INAZUIWA - kunradhi Mhadham Rais, eti ni kutokana na Madrassah zinazoendeshwa humo zinaeneza “ugaidi”?
MKAPA: Kuna mwenye swali lingine?!

Shilingi Milioni Mia Mbili Zaliwa Na ' Panya' Mbarali!
Ndugu zangu,
Juzi usiku kwenye TBC1 iliripotiwa kuwa shilingi milioni mia mbili hazijulikani zilipo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Kamanda wa Takukuru mkoani Mbeya alionekana kwa uchungu kuzungumzia kashfa hiyo huku akiahidi kufanya uchunguzi na kuja na ripoti ndani ya kipindi kifupi. Kamanda huyo alisikitishwa na upotevu huo wa fedha za wananchi.
Kama shilingi milioni mia mbili zinapotea kwenye Halmashauri basi ina maana kuwa kuna ' panya' wanaotafuna fedha za wananchi kwenye halmashauri husika.
Kuna wenye kutakiwa kutolea ufafanuzi zilikokwenda fedha hizo. Wanajulikana. Na kwa vile imethibitisishwa kuwa kuna ' panya' wametafuna fedha za wananchi, basi, hao ni watuhumiwa uhalifu mpaka watakapothibitishwa vinginevyo.
Naam, vihenge ( Vya kuhifadhia mazao) vya WanaMbarali vimeingiliwa na panya. Chonde WanaMbarali, tukicheza na ' panya' waliovamia vihenge vyetu, tutaambulia pumba.
Tunasubiri hatua za vyombo vya dola zitakazofuata.
" I'm Fit For Fight!"- Edward Lowassa
TBC1 usiku huu imeripoti taarifa za ujio wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akitokea Ujerumani. Lowassa alitoa ufafanuzi wa safari yake ya Ujerumani na utata uliotawala juu ya afya yake. Ameweka wazi kuwa afya yake ni safi; hana kisukari wala stroke. Kwamba yuko fit kwa mapambano. Picha kwa hisani ya Kamanda wa Matukio blog.
Mihuri Yadaiwa Kutumika Kuchakachua Matokeo Ya Chaguzi!
ALIYEKUWA Meneja kampeni wa Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Abdulrahaman Kinana, amehusishwa na uchakachuaji wa matokeo ya Ubunge katika Jimbo la Segerea mkaoni Dar es Salaam.
Kinana alidaiwa kuhusika katika uchakachuaji wa matokeo hayo na shahidi wa sita katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo, Livingstone Rugema wakati akitoa ushahidi wake mahakamani jana.
Shahidi huyo alitoa madai hayo kwa nyakati tofauti wakati akitoa ushahidi wake, akiongozwa na wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala na wakati akihojiwa na mawakili wa utetezi, Jerome Msemwa na Wakili wa Serikali (SA) David Kakwaya.
Wakati Kinana akidaiwa kuhusika katika uchakachuaji wa matokeo hayo, Mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Makongoro Mahanga jana aligongana uso kwa uso mahakamani hapo na mpinzani wake Fredy Mpendazoe.
Dk. Makongoro aliibuka mahakamani hapo jana ghafla ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo alisalimiama na Mpendazoe, kisha baadaye wakati akiondoka, akamuomba Mpendazoe afute kesi hiyo ili mwaka 2005 amwachie jimbo hilo.
Kesi namba 98 ya mwaka 2011 inayosikilizwa na Jaji Profesa Ibrahim Juma, ilifunguliwa na Mpendazoe aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akipinga ushindi wa Dk Mahanga.
Wakati Wakili Kibatala akimwakilisha Mpendazoe katika kesi hiyo, Wakili Msemwa anamtetea Dk Mahanga, huku SA Kakwaya akiwatetea Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo ya manispaa hiyo.
Wakati akitoa ushahidi wake na wakati akihojiwa na mawakili hao wa utetezi, shahidi huyo kwanza alidai kuwa yeye alikuwa wakala wa majumuisho wa Chadema katika Kata ya Segerea na kwamba baadaye alikwenda Anatoglou mahali ambako matokeo ya jimbo hilo yalikuwa yakijumlishwa na kutangazwa.
Alidai kuwa wakati wakisubiri matokeo kutangazwa Novemba 2 mwaka 2010 majira ya jioni, Kinana alifika kituoni hapo kisha akaondoka na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo ya Ilala.
Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa matukio yaliyojitokeza baadaye baada ya Kinana kuondoka kituoni hapo Anatoglou, yalitia mashaka kiasi cha kumhusisha Kinana na Mkurugenzi huyo kuwa walikwenda ‘kupika matokeo.’
Shahidi Rugema aliyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na kijana mmoja kukamatwa na mihuri, mtendaji wa Kata ya Tabata, Imelda Kafanabo kukamatwa na fomu za matokeo pamoja na Mtendaji wa Kipawa pia kufika Anatoglou akiwa na fomu peke yake bila mawakala wala polisi.
Alipoulizwa na SA Kakwaya kama wakati wakitoka Kinana na Mkurugenzi aliwaona wamebeba kitu chochote ,shahidi Rugema alijibu kuwa hakuona kitu chochote wala wakati wakiingia hakuwaona.
Lakini alidai kuwa Mkurugenzi aliyeaminiwa kusimamia uchaguzi huru na wa haki, kuonekana akiongozana na mmoja wa wanachama wa vyama vinavyopingana bila kuwepo kwa mawakala wa vyama vingine wala polisi na kwenda mahali kusikojulikana, kilitia shaka.
Alisisitiza kuwa matukio yasiyo ya kawaida yaliyotokea baadaye ikiwamo kukamatwa kwa mihuri na fomu za matokeo na kuonekana kwa watu wasiohusika, inaonesha kuna mahali matokeo hayo yalikwenda kupikwa na kwamba matokeo hayo yaliyotangazwa hayakuwa halali.
“Hata kama alikuwa mmoja wa mawakala wa kura za urais katika jimbo mojawapo (Kinana), lakini kuondoka wenyewe bila mawakala wengine walikwenda kufanya nini? Angetuambia kule walienda kufanya nini na angeongozana na watu wengine,” alisisitiza shahidi Rugema.
Akijibu swali la SA Kakwaya jinsi mihuri hiyo ilivyoweza kuathiri matokeo ya Segerea, shahidi Rugema alidai kuwa kitendo cha mihuri hiyo kuonekana eneo la kujumlishia matokeo na siyo kituo cha kupigia kura, kilifanya uchaguzi huo uonekane si huru na wa haki.
“Hivyo ninaona kuwa matokeo hayo yalipikwa tu. Kulingana na matokeo yaliyokuwa yamebandikwa ukutani Mpendazoe kuna sehemu nyingi alikuwa akiongoza lakini baadaye ikatangazwa kwamba Makongoro ameshinda, naona kuwa mihuri hiyo ndio ilitumika kupika matokeo hayo.
Alidai kuwa katika Kata ya Segerea alikosimamia yeye, majumuisho Mpendazoe alishinda kwa kura 5,496 huku Dk Mahanga akipata kura 3,954.
Shahidi huyo alidai kuwa hata taratibu za utangazaji wa matokeo zilikiukwa kwani matokeo ya kila kituo hayakutangazwa na kwamba hata msimamizi wakati akitangaza matokeo hayo, hakuwa katika hali nzuri huku akiwa chini ya ulinzi mkali.
“Mkurugenzi alipotangaza matokeo hakuwa katika ‘mood’(hali) nzuri kama tuliyozoea kumuona ofisini. Alitakiwa kuonekana mwenye furaha kwenda kumtangaza mshindi kwa zoezi alilosimamia yeye, lakini hakuwa hivyo,” alisisitiza shahidi huyo.
Kwa upande wake Shahidi wa saba, Mwangalizi wa Dawati la Uchaguzi kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC), Merick Luvinga alidai kuwa waliweka waangalizi wa uchaguzi nchini kote na kila kituo katika majimbo 24 yalioonekana kuwa na upinzani.
Alidai kuwa Segerea zilitokea dosari mbalimbali na kwamba waliandika ripoti kwenda Tume ya Uchaguzi iliyosimimamiwa na Profesa Peter Maina, wakipendekeza namna ya kuboresha chaguzi zijazo.
Hivyo aliiomba mahakama imwamini akidai kuwa ana uzoefu wa uangalizi wa chaguzi mbalimbali ndani na nje na kwamba katika ripoti zao, hawajawahi kulalamimikiwa kuwa wamependelea upande mmoja.
Kabla ya kesi hiyo kuanza asubuhi Dk Mahanga alifika mahakamani hapo na kumkuta Mpendazoe ambapo walisalimiana na kisha wakaendelea kusikiliza kesi wakati shahidi wa sita akitoa ushahidi.
Baadaye wakati akitoka nje ili aondoke Dk Mahanga alimkuta Mpendazoe nje ndipo akamwambia katika hali ya utani kuwa aifuete kesi hiyo, ili yeye amalizie muda uliobaki halafu atamwachia jimbo hilo mwaka 2015, lakini Mpendazoe hakumjibu chochote.
Katika kesi hiyo Mpendazoe analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi katika jimbo hilo akida taratibu na sheria za uchaguzi zilikiukwa katika ukusanyaji ujumulishaji na utaratibu wa kuhesabu na utangazaji wa matokeo.
Hivyo anaiomba Mahakama hiyo itengue matokeo ya ushindi wa mbunge aliyetangazwa na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo, au yeye atangazwea mshindi.Chanzo: Gazeti Mwananchi jana Jumatano.

Subscribe to:
Comments (Atom)