Saturday, March 17, 2012

Tendwa: Vincent Alikuwa Mtoto Mno Kujua Kifo Cha Mwl Nyerere


Tendwa alisema, ukweli wa kifo cha Mwalimu Nyerere, anayeufahamu ni daktari wake katika hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyopo Uingereza, ambako mwasisi huyo wa taifa, alilazwa na kupatiwa matibabu mpaka alipofariki
Alisema wakati Mwalimu Nyerere  anafariki , Vincent  alikuwa mtoto mdogo na kwamba taarifa hizo alipaswa kusema Chifu Wanzagi.

“Kwanza nashangaa sana, wakati Mwalimu Nyerere anafariki, Vincent alikuwa mtoto mdogo sana na kwamba hawezi kujua taarifa za kifo hicho labda awe amesimuliwa na baba yake Chifu Wanzagi  ndiye mwenye jukumu la kuzungumzia kifo cha Mwalimu kwa sababu alikuwa kaka yake lakini, huyu ni kijana mdogo sana,” Tendwa alimshukia Vincent.

MY TAKE:
Kwa kauli kama hii inayomshambulia Vincent tena Tendwa alitaka kufanya suluhu au ana lengo lingine? kwani mwaka 1999 Vincent alikuwa mtoto kushindwa kujua kilichotokea kwa baba yao?.Nadhani Tendwa amezidi sasa kufanya propaganda za CCM
Mdau Aliyekereka

No comments:

Post a Comment