MICHEZO

URA FC YA UGANDA YAIFUNGA SIMBA 2-0 UWANJA WA TAIFA
Derrick Walulya mchezaji wa timu ya URA FC kutoka nchini Uganda ambaye aliwahi kuchezea timu ya Simba pia ya Tanzania akimiliki mpira mbele ya Felix Sunzu mshabuliaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kuwania kombe la Kagame linaloandaliwa na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika Mashariki CECAFA unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni hii mpaka sasa mpira umekwisha na timu ya URA imeifunga timu ya Simba magoli 2-0. magoli hayo yamefungwa na mchezaji Feni Ali wa URA FC.
Waamuzi wakiongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.

Watangazaji wa kituoa cha televisheni cha Supersport cha Afrika Kusini wakitoa tathmini ya mchezo huo kabla ya timu hizo kukutana ambapo inaonyesha kuwa Simba mara nyingi imekuwa ikifungwa na URA FC wakati timu hizo zinapokutana katika michuano mbalimbali.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika katika uwanja wa Taifa kujionea timu yao ikicheza na Waganda URA FC.



WAZIRI WA HABARI AMETEUA KATIBU MTENDAJI BAKITA

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara

NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara amemteua Dk. Selemani Sewangi (55) kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa wizara hiyo, uteuzi huo umeaanza rasmi Julai Mosi mwaka huu.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Dk. Sewangi ni Mhadhiri Mwandamizi wa Taasisi za Kiswahili (TATAKI) kutoka Chuo Kikuu cha Dares Salaam.
Dk. Sewangi anachukua nafasi iliyoachwa na Dk. Anna Kishe aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.







Timu zote mbili zikiingia uwanjani

Washabiki wa timu ya simba wakiwa wakifuatilia mpambano huo kati ya timu yao na Al Ahly Shandy
 
Mshambuliaji hatari wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akimtoka  beki wa timu ya Al Ahly Shandy ya Sudani katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa Taifa
Leo wamewatandika Al Ahly Shandy 3-0! Kwao Sudan tunahitaji sare tu, baada ya hapo ni robo fainali.
Simba 3 Na Ahli Shandy 0 Mpira Umekwisha


CHELSEA YAITOA NJE YA MASHINDANO BARCELONA YA HISPANIA
KIUNGO wa Chelsea, Frank Lampard amewapongeza wachezaji wenzake baada ya Chelsea kutoka nyuma mbele ya Barcelona na kushinda kwa jumla ya mabao 3-2 na kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa.

The Blues walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 katika usiku huu kabla ya kumpoteza nahodha wake, John Terry aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwa kumpiga teke Alexis Sanchez.

Lakini bao la kushitukiza la Ramires kabla ya mapumziko lilirejesha matumaini kwa Chelsea kabla ya Lionel Messi kukosa penalti na makosa ya safu ya ulinzi yakampa mwanya Fernando Torres kutimka kwa kasi kwenda kufunga bao lililokamilisha bei ya tiketi ya Chelsea kwenda Munich dakika ya mwisho mchezo.

“Nini kiwango! Najua ngoma ilikwishakuwa ngumu wakati huo, lakini tulipigana hadi mwisho sana," alisema Lampard. “Najua watu walitaka kuona soka maridadi, lakini tukiwa 10 kwa dakika 50 zilizosalia na tukiwa nyuma kwa mabao mawili na kucheza namna ile- tulionyesha morali ya aina gani - ngumu kuamini tulivyoshughulika!

“Saa zilikuwa kama zinakwenda taratibu sana kipindi cha pili, lakini nilikuwa na fikra utakuwa usiku wetu. Wote mnafahamu wanaweza kufunga wakati wowote kwa sababu ya wachezaji wao walionao kwenye timu, lakini kulikuwa kuna kujituma juu yetu.

“Katika mchezo unaopata kile unachostahili na tulikuwa wote wamoja na tulipigana na matunda yake ni matokeo mazuri tuliyopata.”

Lampard alisema hakuwa mwenye kujiamini kwamba mchezo huo ulikuwa salama hadi pale Torres alimpomzunguka Victor Valdes dakika ya mwisho na kuihakikishia Chelsea kutinga fainali dakika ya mwisho ambako watamenyana ama na Bayern Munich au Real Madrid mwezi ujao.

“Niliweza kutulia wakati Fernando alipomzunguka kipa,” alisema Lampard. “Kipindi cha pili kilionekana kama kimechukua muda mrefu - hata zilipobaki sekunde, kilichotokea miaka michache iliyopita walipotufunga bao la ushindi dakika za mwishoni, bado ilikuwa akilini mwetu wote.

“Unashangaa kama ingetokea tena na wakati huo, bahati ilikuwa upande wetu, lakini umeifanya bahati yako mwenyewe na tulistahili matokeo hayo.”

Kiungo huyo alisema hakuona Terry akitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini anampa pole sana Nahodha, ambaye sasa ataikosa fainali.

“Hapana, sikuona tukio hilo," alisema. "John alisema alimkimbilia kwa nyuma. kwa kweli sikuona hilo, lakini nachoweza kusema namfikiria yeye huko huko. Tulikuwa pamoja katika hili na tumeshinda usiku huu, pamoja. kama atakosa fainali na tutaendelea na tutashinda, ambayo ni ombi kubwa, kisha ataibuka na kuungana nasi huko.

“Sitaki hata kufikia nani tutacheza naye kwenye fainali. Real na Bayern ni timu mbili nzuri sana sana, na siwezi kusema tunataka tukutane na nani – ni timu mbili babu kubwa. Ni kweli Chelsea wana heshima kubwa na upendo wa hali ya juu kwa Jose Mourinho baada ya kile alichokifanya hapa, lakini tuko sawa. Hakuna mtu aliyetarajia tungefuzu, hivyo ukweli ni tuko kwenye fainali ni jambo la kujivunia kwetu.”

DIAMOND ASHINDA TUZO TATU KWA MPIGO KILIMANJARO MUSIC AWARD 2012
Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utuzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora za Kilimanjaro Music Award 2012 zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania na nje ya nchi, Diamond amejipatia tuzo tatu kwa mpigo.
Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzni bora wa nyimbo.
Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu.
Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.
Watoto wa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa wakishuka jukwaani mara baada ya kumtunza mama yao wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla hiyo.
Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop
Burudani kutoka THT zikiendelea
Burudani zikiendelea kwa nguzu zote.



PAPIC OUT, TIMBE INN AGAIN YANGA
Aliyekuwa kocha wa Yanga Sam Timbe.
UONGOZI wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga uko mbioni kumrejesha kukinoa kikosi hicho aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mganda Sam Timbe.
Timbe ambaye aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2010/2011 na kombe la Kagame, mkataba wake ulivunjwa msimu uliopita kwa madai ya kushindwa kuiletea mafanikio timu hiyo na nafasi yake kujazwa na Mserbia Kostadin Papic.
Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga zinaeleza kuwa Timbe atarejea kukinoa kikosi hicho wakati wowote kuanzia sasa akirithi mikoba ya Papic.
Imeelezwa kuwa mkataba wa Papic umebakiza siku chache kumalizika na uongozi hauna mpango wa kumuongeza mkataba mkataba mpya,kutokana kutomuhitaji tena.
Mmoja ya viongozi wa Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina lake aliliambia gazeti hili kwamba hawana mpango tena na Papic kutokana na kutokuwa na jipya ndani ya klabu hiyo hivyo wanaendelea na mikakati ya kumrejesha Timbe.
“Mimi nashangaa huyu kocha anazungumza na vyombo vya habari kuwa hajalipwa miezi mitatu, huo ni uzushi ambao hauna maana yoyote...ninachoona ni kutaka kuudanganya umma ili adanganye kuwa kaondoka kwa kutolipwa wakati mkataba wake ulishakwisha,”Aliongeza.
Baadhi ya vyombo vya habari leo viliripoti kocha hutyo kutoambatana na timu Kanda ya Ziwa kutokana na kuugua Tumbo na mafua huku pia ikidaiwa kocha huyo hajalipwa mshahara wake kwa miezi mitatu hali inayomuweka katika mazingira magumu ya ufundishaji wake.
Hata hivyo ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema jana kuwa taarifa za Papic kudai mshahara hazina ukweli wowote na kukiri kuwa kocha huyo ni mgonjwa ndio maana hajaambatana na timu katika safari hiyo , lakini kama hali yake itatengemaa huenda akaungana na timu hiyo leo.
Alisema kikosi cha timu hiyo kinanatarajiwa kuondoka Kahama leo kwenda Mwanza tayari kwa mechi yao ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambapo jumapili kitashuka kwenye dimba la CCM Kirumba, jijini humo kukwaana na wenyeji Toto African.



Tenga Akataa Kujiuzulu Kwa Mohamed






Release No. 050
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 2, 2012
Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amekataa barua ya kuomba kujiuzulu ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Said Mohamed.
Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya Azam alimuandikia Rais Tenga barua ya kujiuzulu wadhifa huo akipinga kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Alfred Tibaigana juu ya adhabu zilizotolewa na Kamati ya Ligi kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga.
Rais Tenga amesema alimteua Mohamed katika Kamati hiyo kwa kuzingatia uadilifu wake na uwezo wake katika kuongoza, hivyo amekataa barua hiyo ya kuomba kujiuzulu.
Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Mkutano Mkuu wa TFF, Rais Tenga, Oktoba 28 mwaka jana aliunda Kamati ya Ligi ambayo wajumbe wake wanatoka kwenye klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza.
Wajumbe wa kamati hiyo ni Wallace Karia (Mwenyekiti), Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti), Damas Ndumbaro, Steven Mnguto, Geoffrey Nyange, Seif Ahmed, Henry Kabera, ACP Ahmed Msangi, Meja Charles Mbuge na Ahmed Yahya.
WASHABIKI 11,056 WASHUHUDIA COASTAL, YANGA
Washabiki 11,056 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Coastal Union na Yanga lililochezwa juzi (Machi 31 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Viingilio katika pambano hilo vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP, sh. 6,000 jukwaa kuu na sh. 4,000 mzunguko. Mapato yaliyopatikana kwenye pambano hilo ni sh. 61,494,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 14,664,927.80 uwanja sh. 4,630,335.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (DRFA) sh. 2,515,494.37.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 4,630,335.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,315,167.97 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 463,033.59.
Nayo mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 29,716,000 kutokana na watazamaji 8,167 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 4,532,949.15, kila timu ilipata sh. 5,031,085.25, Uwanja sh. 1,486,465.08, TFF sh. 1,486,465.08, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,084,600.03, FDF sh. 743,232.54 na BMT sh. 148,646.51.
AZAM, RUVU STARS ZAINGIZA MIL 1.5
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Ruvu Stars lililochezwa jana (Aprili Mosi mwaka huu) Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam limeingiza sh. 1,585,000.
Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 1,000 mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu ni 1,569.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 283,656, uwanja sh. 57,942, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 117,306.08, TFF sh. 57,942, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 28,971 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 5,794.02.


Uchaguzi Babati


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI
WA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA BABATI
TAREHE 27/03/2012
1. Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika kikao chake kilichofanyika tarehe 25 Machi 2012 ilijadili mkanganyiko na mgogoro uliopo wilayani Babati kuhusu uchaguzi wa viongozi wa chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Babati (BDFA).
2. Kamati ilibaini kuwa mgogoro uliojitokeza kuhusu uchaguzi wa BDFA umesababishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Mkoa wa Manyara kwa kutotimiza wajibu wake wa kusimamia uchaguzi wa BDFA na mgogoro wa uongozi ndani ya BDFA uliosababisha kuundwa kwa Kamati mbili za uchaguzi kinyume na matakwa ya Katiba ya BDFA na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini na kujiridhisha pia kuwa, mgogoro kuhusu uchaguzi wa viongozi wa BDFA umepanuka zaidi kutokana na uongozi wa BDFA kutotekeleza maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF yaliyotolewa kwa BDFA na pia Kamati ya Uchaguzi ya MRFA kukaidi maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyoitaka Kamati ya Uchaguzi ya MRFA kusimamisha chaguzi zote Mkoani Manyara ili kuyapatia ufumbuzi mataizo ya uchaguzi yaliyojitokeza Mkoani Manyara.
3. Kwa kuwa Kamati ya Uchaguzi ya MRFA imekaidi kutekeleza maagizo ya TFF kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Katiba ya MRFA na pia kwa kutotimiza kwa makusudi wajibu wake wa kusimamia kwa weledi chaguzi za wanachama wa MRFA na kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa mamlaka yake yaliyoainishwa katika Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya ya 6, Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(6), 26(2) na 26(3) imeamua yafuatayo:
(i) Imefuta na kutengua matokeo ya chaguzi za viongozi wa BDFA zilizofanyika tarehe 19 Februari 2012 na tarehe 11 Machi 2012.
(ii) Imezifuta Kamati za Uchaguzi za BDFA.
(iii) Imeifuta Kamati ya Uchaguzi ya MRFA.
4. Kutokana na maamuzi hayo, TFF inaiagiza Kamati ya Utendaji ya MRFA kuchagua Kamati mpya ya Uchaguzi ya MRFA itakayozingatia matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF katika kutekeleza majukumu yake. Uongozi wa MRFA unatakiwa kuhakikisha kuwa Kamati ya Utendaji ya BDFA inateua Kamati mpya ya uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya BDFA na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF katika Kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe ya barua hii, ili kuanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa BDFA chini ya usimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya MRFA.
Hamidu Mbwezeleni
MAKAMU MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI -TFF

 

Siri Ya Nyota Yanga Kuachiwa Huru Yafichuka

SEKRETARIETI ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inadaiwa ndiyo chanzo cha mkanganyiko wa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliosababisha adhabu za wachezaji wa Yanga kusimamishwa.

Viongozi wa sekretarieti wanadaiwa kubana rufaa ya Yanga kwa kutoiwasilisha kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF iliyokutana wikiendi iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF, Alfred Tibaigana kwa kutumia Kanuni ya 129 ya Kanuni za Adhabu za Fifa aliamuru kusitishwa kwa adhabu zilizotolewa na Kamati ya Ligi ya TFF kwa wachezaji wa timu ya Yanga.
 

Chini ya kanuni hiyo, Mwenyekiti anayo mamlaka ya kusitisha utekelezaji wa adhabu yoyote pale anapoona kwamba ukiukwaji unaolalamikiwa hautaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka bila kuathiri haki za wale wanaokata rufani," ilisema taarifa ya TFF, ambayo inaeleza kwamba Tibaigana amesimamisha adhabu hiyo kwa muda wa siku 14.

Imegundulika kuwa hatua ya Tibaigana kusitisha adhabu hizo ilitokana na sekretarieti kutowasilisha rufaa ya Yanga kwenye kamati hiyo na badala yake waliwasilisha rufaa ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu.

Tibaigana inadaiwa alikuwa amepewa nakala tu lakini barua halisi alikuwa nayo Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni.

Kamanda huyo wa Polisi wa zamani wa Dar es Salaam inadaiwa alipotinga kwenye kikao hicho alihoji kutokuwepo kwa rufaa ya Yanga.

Maofisa wa TFF inadaiwa walimweleza kuwa siku hiyo alitakiwa kusikiliza suala la akina Rage tu na mambo ya Yanga yangepangiwa siku nyingine.

Tibaigana inadaiwa hakukubaliana na kitendo hicho kwa kudai alikuwa na nakala ya rufaa ya Yanga kwa siku nne, ndipo akaamua kutumia Kanuni ya Fifa ili kusimamisha adhabu ya Yanga hadi pale atakaposikiliza shauri hilo.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alikiri kutokea kwa mkanganyiko kwa kufafanua kuwa vielelezo vya rufaa ya Yanga vilikuwa havijaandaliwa kwa kikao cha wikiendi iliyopita.
 
Alichotuagiza ni kwamba, kama tunaamini tuna mashtaka juu ya wachezaji wa Yanga tupeleke pamoja na rufani hiyo, ushahidi, utetezi na kama Yanga nao wana ushahidi wao walete halafu tumweleze Mwenyekiti kuwa kila kitu kiko sawa, alisema Wambura.

Wambura alisema watakaa haraka wiki hii ili kuandaa ushahidi dhidi ya wachezaji wa Yanga na kumkabidhi Tibaigana ili atolee uamuzi.

Wachezaji watano wa Yanga wanakabiliwa na adhabu kutokana na kosa la kumpiga mwamuzi Israel Nkongo wakati wa pambano lao dhidi ya Azam FC.

Beki Stephano Mwasika alifungiwa mwaka mmoja, Jerrson Tegete (miezi sita), Nadir Haroub Canavaro' (mechi sita), Omega Seme na Nurdin Bakari mechi tatu kila mmoja. Pia walipigwa na faini.

Naye Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesiga aliiambia Mwanaspoti kuwa soka duniani kote inaendeshwa kwa sheria na kanuni na endapo kanuni hizo zinashindwa kufuatwa basi ni kosa.
 
Tibaigana yuko sahihi kabisa kwani amefuata kanuni zinavyosema, baada ya ile mechi tulikata rufaa lakini haikusikilizwa na Kamati ya Ligi ilikurupuka na kutoa uamuzi wa kuwafungia wachezaji wetu, kitu ambacho kilitushangaza kwani haina uwezo huo.
 
Si sahihi Kamati ya Ligi kusikiliza na kuamua masuala ambayo si mahala pake, kamati hiyo inahusika na hukumu iliyotolewa na refa tu ndani ya uwanjani, lakini yale matukio mengine haihusiki nayo bali Kamati ya Nidhamu ndiyo ilipaswa kutolea uamuzi.
 
Mtu hata kama anapata adhabu iwe kwa haki kutokana na taratibu kufuatwa, hivyo kama Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi itaamua baadaye lolote, hapo ndipo tunaweza kukubali au tutaangalia kinachotokea, alisema Mwesiga.






KOMBE LA UEFA KUKANYAGA BONGO MACHI 26

BIA ya Kimataifa ya Heineken imetangaza
udhamini wa ziara ya Kombe la Mabingwa wa Ligi ya Ulaya (UEFA) 2012 katika Afrika Mashariki, ambako litakuwa jijini Dar es Salaam Machi 26 na 27.
Meneja Uhamasishaji wa Heineken, Hans Erik Tuijt, alisema, Heineken, imekuwa na uhusiano na Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, tangu msimu wa 2005/06 na itabakia kuwa moja ya wadhamini wakuu wa ligi hiyo hadi msimu wa 2014/15.
Alisema, ziara hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki, itaanzia Nairobi hadi Dar es Salaam kupitia Mombasa na baadaye kurudi Nairobi na kisha kuelekea Shanghai, China, ambako kwa kipindi hicho, wateja watakaonunua bia hiyo, watazawadiwa tiketi ya kwenda kwenye matukio ya kipekee ya kombe hilo na kupata fursa ya kuona uzoefu wa kandanda.
Tuijt alisema; “Kila msimu wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Heineken inajitahidi kuwa na mazungumzo na mashabiki. Uzinduzi wa ziara hii ya Kombe la Mabingwa wa Ulaya kwa mwaka huu, unawaletea karibu mashabiki wa mpira wa miguu duniani, kwa tukio ambalo litawawezesha kujumuika na Heineken kwenye mashindano na wakati tunakaribia kwenye fainali, tutashirikiana na mashabiki ili kuonesha uzoefu wa kihistoria,”.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Matukio wa UEFA, David Taylor, alisema, Ligi ya mabingwa UEFA, ina urithi wa muda mrefu na ni nguzo ya soka la klabu za Ulaya. Ziara ya Kombe hili, kimsingi inaelezea ukweli wa jinsi ilivyokubalika duniani na mwitikio uliopo kwa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya.

SIMBA WAITUNGUA MTIBWA SUGAR 2-1, AZAM WATEREMSHA YANGA


MABAO ya ‘ma tx’ kiungo wa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango dakika ya 18 na mshambuliaji wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya 74, jioni ya leo kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro yameiwezesha Simba SC kukalia kwa madaha- kwa kujinafasi kiti cha uongozi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuibwaga Mtibwa Sugar 2-1.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Hussein Omar Javu aliifungia Mtibwa bao lililokuwa la kusawazisha dakika ya 52, ambalo mwisho wa mchezo lilikuwa la kufutia machozi- kufuatia Sunzu kutupia la ushindi kwa Simba.
Ushindi huo, unawafanya Wekundu wa Msimbazi watimize pointi 47- wakiwaacha kwa pointi nne mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 43 katika nafasi ya tatu.
Azam jana ilirudi nafasi ya pili kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi, Mbagala jioni ya leo, bao pekee la Mrisho Khalfan Ngassa.
Ushindi huo, unaifanya Azam sasa itemize pointi 44, ingawa imecheza mechi moja zaidi ya mabingwa watetezi, wakati Simba nayo pia imecheza mechi moja zaidi ya wapinzani wao wa jadi, Yanga.




Mwape wa yanga akijaribu kumfunga Juma Kaseja, Yanga leo anashuka dimbani kuvaana na klabu ya Villa Squad
MABINGWA watetezi, Yanga leo watarudi kwenye nafasi yao ya pili kama watafanikiwa kuichapa Villa Squad katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ina pointi 40 baada ya kucheza michezo 19, ikiwa nyuma ya Azam kwa pointi moja na nne kwa vinara wa ligi Simba wenye pomti 44, ambapo Azam watashuka dimbani kesho kuikabili Ruvu JKT  huku Simba ikicheza na Mtibwa Sugar.

Pamoja na Yanga kuwapoteza nyota wake kadhaa, katikati ya wiki hii ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon na kurudisha matumaini yao kwamba wanaweza kutetea taji lao.

Mabingwa hao watetezi wataingia uwanjani wakiwa na tumaini la kuendeleza kasi ya ushindi dhidi ya vibonde wa ligi Villa Squad yenye pointi 16 ambayo inaonekana kama imekubali kushuka daraja msimu huu.

Kocha wa Villa, Habibu Kondo alisema wao wana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mechi ya leo kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya.

"Hatuwaogopi Yanga na tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo kama ilivyokuwa kwa Simba," alisema Kondo.

Villa Squad iliwashangaza watu mwaka huu pale ilipowafunga Simba bao 1-0 ukiwa ni moja ya ushindi wake wa nne katika mechi 19 ilizocheza msimu huu.

Nahodha wa Villa, Nsa Job atakuwa na kazi moja ya kuhakikisha anawaongoza wenzake kuifunga timu yake ya zamani ya Yanga ili kufufua matumaini yao ya kubaki Ligi Kuu.

Pamoja na kushikilia mkia, Villa imefanikiwa kufunga mabao 20 wastani wa bao moja kwa mechi huku nahodha wao Job akiwa amezifumania nyavu mara nane.

Ubora huo wa safu ya ushambuliaji wa Villa ni kitu ambacho kocha Kostadin Papic wa Yanga anapaswa kuutafakari na kuangalia upya ukuta wake ulioruhusu mabao 16 wavuni msimu huu.

Kurejea kwa kiungo Haruna Niyonzima katika mechi hii kumetoa faraja mpya kwa kocha Papic.

Niyonzima atakuwa na jukumu moja la kuwatengenezea nafasi washambuliaji wake Kenneth Asamoah na Davies Mwape na kuna shaka kwamba wataendelea kusababisha maafa kwa ngome ya Villa iliyoruhusu mabao 40.

Kwa mara nyingine Shirikisho la Soka Tanzania TFF, limemteua mwamuzi Oden Mbaga mwenye beji ya Fifa kuchezesha mechi ya Yanga katika kipindi cha siku nne.

Mwamuzi Mbaga ndiye aliyechezesha mechi ya Jumatano iliyopita wakati Yanga iliposhinda 1-0 dhidi ya Lyon.

Mechi nyingine ya leo itachezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, ambapo Coastal Union watakuwa wenyeji wa Oljoro JKT ya mkoani Arusha.

Ligi itaendelea tena kesho kwa mechi mbili wakati vinara wa ligi Simba watakapokuwa wageni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Azam watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Stars kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Simba na Azam zitaingia uwanjani kwa lengo moja la kupata ushindi na kuendelea kubaki katika nafasi mbili za juu.

Simba pia watautumia mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kama sehemu ya maandalizi yao ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya ES Setif ya Algeria utaofanyika wiki ijayo. 





Uharibifu Wa Viti Uwanja Wa Taifa




Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Machi 14 mwaka huu) limepokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu uharibifu uliofanyika kutokana na vurugu za washabiki wa Yanga kwenye mechi dhidi ya Azam.

Kwa mujibu wa tathmini ya Serikali, katika vurugu hizo kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jumla ya viti 119 viliharibiwa. Gharama za uharibifu huo ni sh. milioni 5 ambazo Serikali imeagiza zilipwe mara moja.

Kwa vile washabiki wa Yanga ndiyo waliohusika na vurugu na uharibifu huo, gharama hizo zitabebwa na klabu hiyo ili Serikali iweze kufanya ukarabati haraka.

TFF inarudia tena kulaani na kukemea vurugu zinazofanywa na washabiki viwanjani na kusababisha usumbufu, uvunjifu wa amani na uharibifu wa vifaa hasa kutokana na ukweli kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa burudani.

Tunapenda kuwakumbusha washabiki na klabu kuwa vitendo hivyo si vya kistaarabu, hivyo havikubaliki katika mpira wa miguu, na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa wahusika iwapo vitaendelea kutokea viwanjani.

TENGA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI LEO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kesho (Machi 15 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ofisi za TFF.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Mpira Wa Miguu Kuadhimisha Siku Ya Wanawake

Release No. 034
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 7, 2012

MAKONGO, LORD BADEN KUCHEZA FAINALI
Shule ya Sekondari ya Makongo ya Dar es Salaam na Lord Baden ya Bagamoyo mkoani Pwani ndizo zitakazocheza fainali ya mashindano maalumu ya mpira wa miguu kwa wanawake kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Fainali hiyo itachezwa kesho (Machi 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Karume kuanzia saa 10 kamili jioni. Michuano hiyo ilianza Februari 24 mwaka huu ikishirikisha timu nane za shule za sekondari.

Michuano hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA).

Kundi A lilikuwa na shule za Makongo, Goba, Twiga na Lord Baden ambapo zilichezea mechi zake za awali katika uwanja wa Sekondari ya Makongo. Timu zilizounda kundi B na kuchezea mechi zake uwanja wa Shule ya Sekondari Jitegemee ni Benjamin Mkapa, Jitegemee, Kibasila na Tiravi.

Lengo lingine la mashindano ni kuhamasisha mpira wa miguu kwa wasichana katika ngazi ya shule, kuandaa, kubaini na kuendeleza mafanikio yanayopatikana katika timu ya wanawake ya Taifa.

Uchaguzi wa timu shiriki ulizingatia mchango wa shule katika kuendeleza mpira wa miguu kwa wasichana/wanawake. Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo ni Zainab Mbiro kutoka Twiga Sekondari.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)



SIMBA YAITUNGUA TIMU YA KIYOVU TOKA RWANDA 2-1

Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi kulia akijaribi kumtoka mchezaji wa timu ya Kiyovu ya Rwanda wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho katika ya timu hiyo na Kiyovu ya Rwanda unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Simba imefanikiwa kuiondosha Kiyovu ya Rwanda magoli 2-1, magoli ya Simba yamepatikana katika kipindi cha kwanza na yamefungwa na mshambuliaji Felix Sunzu akipokea pasi nzuri, kazi iliyofanywa na mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba. Timu ya Kiyovu imefanikiwa kupata goli lake la kwanza katika kipindi cha pili cha mchezo huo, hata, Simba imefanikiwa kusonga mbele katika mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,
Wachezaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wakishangili mara baada ya mchezaji Felix Sunzu kufunga goli la pili kati ya magoli mawili aliyofunga
Timu zikiingia uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo huo jioni hii.
Mashabiki wa Simba wakishangilia kwelikweli wakati timu hizo zikicheza.
Kulikuwa n a kila shamrashamra kwa mashabiki wa Simba kama unavyowaona katika picha.
Hii inaashiria kwamba kama matokeo yatakuwa hivihivi mana yake ni kwamba Simba itaendelea kukwea Mwewe yaani Ndege kwa ajili ya kushiriki raundi ya pili ya michuano hiyo.

Ndoa imevunjika
Roberto Di Matteo
Habari moto moto kutoka mtandao wa klabu ya Chelsea inayocheza katika Ligi kuu ya England,zasema kua klabu hio imeachana na kocha Andre Villas-Boas leo jumapili.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 34 amepoteza kazi hio saa 24 baada ya kupoteza jana pambano la Ligi dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion 1-0.
Kufuatia mechi ya jana Chelsea ilijikuta katika nafasi ya tano kweenye msimamo wa Ligi.
Tangazo la Chelsea limesema kua aliyekua naibu wa Kocha huyo Roberto Di Matteo atashikilia wadhifa wa Kocha hadi mwisho wa msimu
Source:BBC 









Kitaeleweka Rooney ajipanga kutoa maangamizi
Wayne Rooney
LONDON, ENGLAND
WAYNE Rooney, ambaye kikosi chake kitapambana na Tottenham leo Jumapili, amesema ana uhakika kuwa watapata ubingwa wa Ligi Kuu England kwa sababu wachezaji wa Manchester United hawana kawaida ya kuchanganyikiwa.

Manchester United imerudi katika kiwango katika siku za karibuni ambapo mwezi uliopita walitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kutoka sare ya mabao 3-3 na Chelsea huko Stamford Bridge na wiki iliyopita waliifunga Norwich mabao 2-1. Rooney anasema anaamini wataendelea kufanya vizuri zaidi.

Lakini Rooney anaongeza kuwa hakuwa na imani hiyo wakati alipojiunga Manchester United mwaka 2004.
Wakati nilipohamia katika klabu hii nikiwa na umri mdogo nilikuwa napata mashaka wakati tunapofungwa. Lakini sasa nimekuwa mtu mzima, nina uzoefu wa kutosha, tunapofanya makosa, huwa hakuna sababu ya kuchanganyikiwa bali tunapata ari zaidi.

Kujiamini huku kunatokana na kucheza mechi nyingi na kupata uzoefu wa kutosha.
Lakini, Manchester United ilikuwa na wakati mgumu wiki iliyopita wakati ilipolazimika kusawazisha bao dakika ya 83 kwenye mechi dhidi ya Norwich na baadaye wakapata bao la ushindi dakika za lala salama kupitia kwa Ryan Giggs na kuendelea kuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi mbili.

Nyota huyo mwenye miaka 26 amesema mechi dhidi ya Chelsea ilitosha kuionyesha Manchester City kwamba wanaweza kufanya maajabu wakati wowote.

Kila mtu aliyeangalia mechi hiyo alifahamu kuwa huwa hatukati tamaa, huwa tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata pointi muhimu.

Wakati timu nyingine zinapokuwa nyuma kwa mabao 3-0 hukata tamaa na hujipanga kuzuia mabao mengine yasifungwe, alisema.

Rooney atakuwemo katika kikosi kesho Jumapili baada ya kukosekana katika mechi dhidi ya Norwich na mechi ya kirafiki kati ya England na Uholanzi.

Tunatakiwa kucheza kwa umaniki ili kupata ushindi, alisema.

Watani Zangu Poleni Sana
Timu ya Yanga kutoka Tanzania imepata kichapo cha goli moja kwa bila na timu ya Zamalek ya Misri leo , katika mchezo uliofanyika nchini humo jioni ya jana ikiwa ni michuano ya Klabu Bingwa Afrika, wiki mbili zilizopita hapa jijini Dar es salaam Zamalek iliilazimisha Yanga kwa kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa |Taifa kwa matokeo ya leo ina maana Zamalek imeifunga Yanga magoli 3-1 na kuitupa nje ya mashindano hayo.

Yanga kikaangoni Cairo leo


Kocha wa Yanga,Kosta Papic

MABINGWA wa Tanzania, Yanga wanaingia dimbani leo wakiwa na lengo la kuvunja mwiko wa kufungwa na timu za kaskazini watakapoivaa Zamalek kwenye Uwanja wa Chuo cha Jeshi majira ya saa 12 jioni sawa na saa moja usiku za Tanzania.

Katika mechi hii ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inahitaji sare ya mabao 2-2 kusonga mbele au ushindi wowote kutokana na matokeo ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza mjini Dar es Salaam, lakini suluhu au sare ya bao 1-1 ni nzuri kwa Zamalek.

Pamoja na ndoto hiyo wachezaji wa Yanga wanapaswa kusahau hali ya hewa ya baridi ambapo leo inatarajiwa kufika nyuzi joto 13 -14 wakati mechi hiyo itakapokuwa ikichezwa.

Pamoja na hali hiyo kocha wa Yanga, Kostadin Papic leo atalazimika kuendelea kutumia mfumo wake wa 4-3-3 na kuhakisha anapata bao la mapema litakalomwezesha kukaa kwenye mazingira mazuri ya kufuzu.

Hakuna shaka safu ya ushambuliaji wa Yanga itaanza na washambuliaji Davies Mwape, Asamoah na Hamis Kiiza akitokea pembeni huku Jerryson Tegete akiwa benchi.

Kutokana na kelele za mashabiki na viongozi wa Yanga, kocha Papic aanaweza pia akampa Tegete kuthibitisha ubora wake mbele ya ngome ya Zamalek.

Safu ya kiungo itaongozwa na Haruna Niyonzima akipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Nurdin Bakari aliyekuwa majeruhi pamoja na Juma Seif 'Kijiko' katika kuhakikisha wanavuruga mipango yote ya Zamalek.

Kurejea kwa Ahmed Hossam ìMidoî aliyekuwa nje kwa miezi miwili na kiungo Mahmoud Abdul-Razek 'Shikabala' kwa Zamalek kutamlazimisha kocha Papic kutoa mbinu mpya kwa ngome yake.

Nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na beki wa kushoto Stephan Mwasika bado hawaonyeshi kiwango cha kuvutia tangu waliporejea baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Mabeki wa kati Nadir Haroub na Athuman Idd watakuwa na jukumu moja kubwa la kuhakikisha mshambuliaji Razak Omotoyossi na Mido hawachezi mipira yote ya krosi kutoka kwa Shikabala.

Haki za matangazo ya mchezo huo zimenunuliwa na klabu ya Al Ahly mwezi mmoja uliopita uliopita.

BARIDI

Kocha Papic amesema wameanza kuzoea hali hiyo na hawana jinsi kwani inabidi kukabiliana nayo, ingawa usiku hali ya hewa hubadilika na kutesa zaidi.

Papic alisema hawana wasiwasi na wako tayari kwa lolote na kama itabidi wachezaji watavalishwa glovus ila hapendi suala la hali ya hewa likuzwe sana kiasi cha kuchanganya wachezaji ingawa amekiri ni tatizo ila hawana jinsi tena.

Wachezaji wamelalamika baridi huku baadhi yao akiwamo Kenneth Asamoah wakiomba watafutiwe glovus ili kuendana na hali ya hewa na baridi hususani leo saa 12 jioni watakapocheza.

"Naomba nitafutie glovus zozote nyepesi utakapokuja nitakulipa," alisikika Asamoah akimnong'oneza Afisa mmoja wa ubalozi wa Tanzania mjini hapa anayeshughulika na Yanga.

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro alisema,"Sisi tunaokaa pale kwenye benchi sijui itakuwaje hiyo baridi ni kali sana halafu usiku upepo unachapa sana kwenye miguu."

UWANJA
Uwanja wa Chuo cha Jeshi ulioko nje kidogo ya Jiji la Cairo una uwezo wa kuchukua mashabiki 22,000, lakini leo utakuwa mweupe  kutokana na CAF kuifungia Zamalek.

Watanzania wanaoishi mjini hapa wamedai huenda kukawa na idadi kubwa ya askari ambao watakuwa kama walinzi, lakini wakitoa msaada kwa wenyeji washinde.

Katika Uwanja huo wa jeshi inaelezwa kuwa mashabiki huwa hawapendi kwenda kutokana na ulinzi mkali mno wa wanajeshi ambao hauwaruhusu kupiga mafataki na makelele yao ndani ya mazingira hayo.

Wanachama mbalimbali wa Yanga waliosafiri hadi hapa wakiongozwa na mwanachama mashuhuri wa Yanga, Wampunga wamekuwa wakihaha kuhakikisha kambi inakuwa salama na wachezaji hawagusi kitu chochote bila idhini ya viongozi wao ingawa wamekuwa wakiwakataza kuzungumza na vyombo vya habari vya Misri.

Kikosi cha kwanza huenda kikawa hivi; Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Stephan Mwasika, Athumani Idd 'Chuji', Nadir Haroub, Juma Sefu 'Kijiko', Nurdin Bakari, Haruna Niyonzima, Kenneth Asamoah/Jerryson Tegete, Davies Mwape na Hamis Kiiza. 


United kwa Spurs, Arsenal yaitesa Liverpool

MANCHESTER, England,
MANCHESTER United watafuta kabisa ndoto ya Tottenham Hotspur kutwaa ubingwa kama wakishinda jijini London kesho na kuacha mbio za ubingwa kubaki kwa timu za kaskazini magharibi mwa England.

Vijana wa Alex Ferguson watashuka kwenye Uwanja wa White Hart Lane kesho kuwavaa majeruhi Spurs, ambao ndio kwanza wameanza kujijenga upya baada ya kupokea kipigo cha mabao 5-2 wiki iliyopita kutoka kwa mahasimu wao Arsenal, matokeo yaliyowafanya kuwa nyuma kwa pointi nane kwa United inayoshika nafasi ya pili.

Naye kocha Spurs, Harry Redknapp amesema kumaliza nafasi ya tatu kwao yatakuwa mafanikio makubwa msimu huu, mshambuliaji Emmanuel Adebayor amegoma kukata tamaa ya kusaka ubingwa kwa kuziachia timu mbili za Manchester.

United hajafungwa na Spurs tangu Mei 2001 na Ferguson amesema kuilinda rekodi hiyo ndiyo siri ya mafanikio yao msimu huu.

ìItakuwa mechi ngumu,î alisema bosi huyo wa United. ìKama tukiweza kupita hapo, itakuwa ni hatua kubwa, kwetu kuelekea kutimiza ndoto yetu ya kutwaa ubingwa wa ligi.î

Mabingwa hao watetezi wanapointi 61 katika michezo 26 na wapo nyuma ya vinara Manchester City kwa tofauti ya pointi mbili.
Timu hiyo ya Roberto Mancini watakuwa wenyeji wa timu ya pili kutoka mkiani Bolton Wanderers leo mchezo unaowapa nafasi ya kuwa mbele kwa pointi tano kabla ya mechi ya United hapo kesho.

Ferguson tayari anafikiria kuhusu mechi ya April dhidi ya City, kuwa ndiyo itakayoamua nani atakuwa bingwa na kupambwa na maua ya rangi blue au nyekundu.

Nataka kwenda hapo nikiwa na pointi sawa,î alisema. ìLakini kama tukienda hapo kwa hatua hiyo wote tukiwa kileleni, tutaweza kuchukua taji.î

ONYESHA UBORA  
Spurs, itashuka dimbani bila ya kiungo wake Scott Parker baada ya kuonyesha kadi nyekundu dhidi ya Arsenal, lakini Adebayor anaamini ushindi wa kesho utawapa matumaini ya kutafuta ubingwa.

Kama unataka kuwa bingwa lazima ucheze mechi dhidi ya Manchester United na mechi kama hizi ndizo unazotakiwa ushinde,î aliimbia Spurs TV.

Baada ya kufungwa 5-2 na Arsenal hatuwezi kujiuliza tena zaidi ya kucheza mechi ngumu dhidi ya Manchester United, lakini tumejiandaa kwa mchezo huuÖTunatakiwa kuonyesha ubora wetu na kujiamini na kurudi kwenye mstari wa ushindi haraka.î

Kipigo cha Spurs kitatoa nafasi kwa Arsenal na Chelsea kuwania nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

Timu zote zina pointi 46, huku Arsenal wakishika nafasi ya nne mbele ya Chelsea kwa tofauti ya mabao.

Arsenal wanakibarua kigumu leo mbele ya Liverpool, timu iliyotoka kumaliza ukame wa mataji wa miaka sita baada ya kunyakuwa ubingwa wa Kombe la Ligi wiki iliyopita siku ambayo Gunners pia walipata ushindi mnono dhidi ya Spurs.

Arsene Wenger alisema timu yake ìipo kwenye kiwango cha juu kuliko watu wanavyofikirî na inaweza kuwaondoa wapinzani wao wa kaskazini mwa London katika kufuzu moja kwa moja kwa Ligi ya Mabingwa kama wakiendelea kucheza kwa kiwango waliochoonyesha mwishoni mwa wiki.

Chelsea watakuwa wageni wa West Bromwich Albion leo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bolton waliopata wiki iliyopita na kocha Andre Villas-Boas akiwa kwenye kitimoto cha kuhusu mstakabali wake.

Michezo mingini wiki hii itazikutanisha Newcastle United watakuwa nyumbani kuikaribisha Sunderland  kesho.



VILLAS-BOAS: LAMPARD SIO MKE WANGU SIHITAJI KUPATANISHWA NAE.
Bosi wa Chelsea Andre-Villas Boas amesisitiza hakuna haja kupatana na Frank Lampard huku akitania “Hatujaoana.”
Lampard wiki iliyopita alikiri kwa mara ya kwanza kwamba mahusiano yake na AVB sio mazuri, lakini AVB amesema haoni umuhimu wa yeye kukaa na chini na Lampard kumaliza tofauti zao, huku akisisitiza bado wanazungumza wanapokuwa mazoezini.
“Mwisho wa siku ni mahusiano kati ya kocha na mchezaji, maneno ya Frank ni ya kweli kutokana na mahusiano yetu yalivyo.
“Kwangu mimi nakubaliana na aliyoyasema, sina tatizo lolote.”
Lampard ameweka wazi kwamba hana furaha na idadi ndogo ya michezo aliyopewa msimu huu lakini AVB alisema: “Inanibidi kuchagua timu – kuchagua timu iliyo bora kwa kila mechi.
“Frank amekuwa hapati sana nafasi lakini haimanishi kwamba nina matatizo nae binafsi.”


Hiki ndio kikosi cha timu ya simba kilichoitoa na kuivua ubingwa klabu ya zamalek mwaka 2003  kwenye michuano ya kombe la mabingwa wa afrika. ilikuwa ndio mara ya kwanza na mwisho kwa timu ya Tanzania kushinda katika ardhi ya Misri.

 Yanga kesho wanacheza na Zamalek inabidi na inapaswa wajitume na kuhakikisha wanaifikia rekodi ya watani wao wa jadi kwa kuwatoa Zamalek tena wakiwa nyumbani kwao Misri na kuweza kuiletea sifa nchi na maendelea ya mpira bongo kwa ujumla.
UONGOZI wa klabu ya Simba leo unaingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Etech kwa ajili ya kufungua tovuti (website) itakayokuwa ikitoa taarifa zote zinazoihusu klabu hiyo.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa wameamua kuingia mkataba ili wapenzi wa timu hiyo wapate habari kwa uharaka kupitia tovuti hiyo baada ya ile ya mwanzo kutofanya kazi katika kiwango kizuri na kuamua kuifunga.

Alisema kupitia tovuti hiyo uongozi wa Simba unaamini wapenzi wa klabu hiyo watapata habari zinazohusu timu hiyo kwa uharaka zaidi na kwa muda wowote sambamba na kutoa maoni yao juu ya maendeleo ya timu yao.

"Kuanzia Machi 1 Simba itaingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Etech, ambapo itafungua tovuti kwa ajili ya kupata habari za klabu yetu kwa uharaka na kwa muda unaotakiwa, lengo hasa ni kurahisisha mawasiliano kati yetu na wadau wetu, ambapo tutakuwa tukienda kisasa zaidi,"alisema Kamwaga.

Wapinzani wa vinara wa Ligi kuu ya Vodacom Simba SC katika michuano wa kombe la shirikisho CAF, Kiyovu SC wanataraji kuwasili kesho badala ya leo.

Kiyovu ilitarajiwa kuwasili leo jioni lakini kutokana na kukosa ndege watakuja nchini kesho kwa ajili ya mchezo wa marejeano, utakao chezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa awali uliochezwa katika jiji la Kigali ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya goli 1-1. Goli la Simba likifungwa na Mwinyi Kazimoto.

Katika hatua nyingine Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuwasili nchini kesho na kujiunga na kambi ya Simba moja kwa moja. Okwi alikuwa na timu ya taifa ya Uganda iliyofungwa goli 3-1 na Congo.

Wakati huo huo Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wamewasili salama jijini Cairo, kwa ajili ya mchezo wa marejeano dhidi ya Zamalek, mchezo utakao chezwa katika uwanja wa jeshi bila ya mashabiki.

Vilevile na Jamhuri ya Pemba nayo iliwasili salama nchini Zimbabwe, ambapo wanataraji kucheza na Hwange ya Zimbabwe, baada ya kuchapwa goli 3 katika mchezo wa awali wa kombe la shirikisho CAF uliochezwa katika uwanja wa Gombani.

Wawakilishi wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo FC wao watasafiri machi 7 kwenda Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa marejeano.



Hii Ni Sawa Kupokea Kombe La UEFA?

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga picha na Kombe hilo pamoja na mawaziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Dk Fenella Mukangara, wa pili kutoka kushoto ni Dk Emmanuel Nchini Waziri wa wizara hiyo na Makamu wa kwanza wa shirikisho la mpira miguu nchini Tanzania (TFF) Athuman Nyamlani

 

MESSI AFANYA KWELI, SASA NDIYE GWIJI WA MABAO BARCELONA

MUARGENTINA Lionel Messi sasa ndiye mfungaji bora wa kihistoria wa Barcelona.
Mshambuliaji huyo ameweka jina lake katika historia za kudumu za klabu hiyo baada ya usiku huu kupiga mabao matatu peke yake na kutimiza mabao 234 hivyo mfungaji nambari moja milele wa klabu hiyo.
“Tuko nyuma ya mchezaji bora hakika kwa kila namna,” alisema kocha wa Barcelona, Pep Guardiola. “Anastahili kwa kila kitu ambacho mwanasoka anatakiwa kufanya na amefanya hivyo kila baada ya siku tatu.
Messi alifunga hat trick yake ya 18 kihistoria akiwa na klabu hiyo ya Catalan na kuvunja rekodi ya gwiji wa klabu hiyo, Cesar Rodriguez aliyefunga jumla ya mabao 232 iliyodumu kwa miaka 57, na kuingia kwenye orodha ya magwiji wa kihistoria waliofanya mambo makubwa kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Wakati Cesar aliweka rekodi hiyo ndani ya miaka 13 kuanzia msimu wa 1942 hadi 1955, kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, Messi amehitaji misimu minane tu kufa nya mambo hayo adimu.
Messi alifunga mabao hayo katika ushindi wa kwenye mechi ngumu kuliko ilivyotarajiwa wa mabao 5-3 dhidi ya Granada, mechi ambayo timu yake ilikuwa lazima ishinde kama inataka kuweka hai matumaini ya kutwaa taji la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Muargentina huyo aliunganisha krosi ya Isaac Cuenca dakika ya 17 na kufikia rekodi ya Cesar, na kasha akapiga mawili zaidi kwa pasi za Dani Alves kuipatia ushindi timu yake, baada ya Granada kusawazisha na kupata 2-2.
Messi, mwanasoka bora wa dunia mara tatu, sasa amefikisha mabao 54 kwenye mashindano yote msimu huu, yakiwemo ya rekodi katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa, matano wiki mbili zilizopita.
Wakati wote safu ya ulinzi ya wapinzani huwa na mchecheto juu yake, Messi amethibitisha yeye hazuiliki, akifunga mabao 17 katika mechi saba mfululizo.
Hat trick yake katika mechi na Granada inamfanya sasa awe anaongoza kwa mabao kwenye La Liga, akimzidi mawili mpinzani wake mkubwa, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Ushindi huo wa sita mfululizo kwa Barcelona, unapunguza idadi ya pointi ambazo wanazodiwa na vinara wa La Liga, Real Madrid hadi kubaki tano, ingawa wapinzani wao Jumatano hii wanashuka dimbani na Villarreal.
Barcelona awali ilikuwa inaamini kwamba Cesar amefunga mabao 235 ndania ya misimu 13 kati ya 1942 na 1955, lakini baada ya kurudia kupitia makabrasha yan historian a rekodi kwa pamoja na gazeti la La Vanguardia, wakagundua walimuongezea Cesar mabao matatu.
Messi amefunga mabao 153 katika ligi ya Hispania, 49 katika Ligi ya Mabingwa, 19 katika Kombe la Mfalme, nane katika Super Cup ya Hispania, manne katika Klabu Bingwa ya Dunia na moja kwenye Super Cup ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment