Vicent Nyerere amemlipua Msajili wa Vyama vyaSiasa,
John Tendwa, kwa kumzuia kumzungumzia Hayati Mwalimu Nyerere.
Amemshauri kuwa kama anahitji kuwa mmoja wa familia
yao, anaruhusiwa kuandika barua kuomba kujiunga na ukoo wao kama alivyofanya
Mkapa.
Alisema anamshangaa Tendwa kumpiga marufuku kuongelea
mambo ya baba yake na kulidanganya Taifa kuwa watahatarisha amani nakujenga
chuki kwa Taifa kwa kumzungumzia Nyerere.
“Mimi huyu ni baba yangu na kila siku lazima nimtaje na
sisi wakatoliki tuna sala maalum ya kumwombea Nyerere na leo (jana) pia nimesali
mara baada ya kuamka, sasa yeye ni nani anayenizuia kutaja jina lababa yangu,
kama anataka ajiunge na ukoo wetu aombe kwa barua, kama alivyofanya mwenzake
Mkapa, aliandika barua akaingizwa katika ukoo,”alisema Nyerere.
Akimnadi Nassari katika mkutano wa hadhara wakampeni,
Vincent Nyerere, ambaye ni Meneja wa kampeni za mgombea ubunge waChadema Jimbo
la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, jana alisema kuwa Mkapa amemfuata Joseph
Butiku kuomba amuombea msamaha kwake (Vincent). Alisema kuwa Mkapa alimweleza
Butiku kuwa alikuwa anamtania ingawa mbunge huyo aliichukulia kauli ya Rais huyo
mstaafu kama ya kweli.
“Huyu Butiku jana (juzi) alinipigia simu akiniomba
tuachane na haya mambo ya malumbano kwa sababu Mkapa alikuwa ananitania na
hakujua kama itakuwa hivyo, na mimi nimeendelea kulisema hadharani, sasa anaomba
basi yaishe,”alisema Nyerere katika mkutano uliofanyika katikakijiji cha Msitu
wa Mbogo, Kata ya Mbuguni.
Alisema kuwa amekataa kuombwa radhi kupitia njia yasimu
au kukutana wawili na kuongeza kuwa anachotaka ni Mkapa kwenda Arumeru kuomba
radhi katika mkutano wa hadhara ambao aliuhutubia na kumchafua kuwa hanaundugu
na Hayati Mwalimu Nyerere.
Aidha, alisema Mkapa anapaswa kuwenda kumuomba radhi
kwenye ukoo wao. “Mimi ni wa ukoo wa Nyerere atake asitake, Nyerere ni baba
yangu na sitaacha kumtaja kamwe,” alisema Vincent.
Alisema kuwa Mkapa alikuwa anamheshimu sana kama Rais
mstaafu na alifahamu anahitaji kupumzika, ila kwa kumgusa kwa hilo nakumchafua
hadharani kuwa anajifanya mtoto wa Nyerere, wakati hamfahamu, kwa hilo aende
katika ukoo kumsafisha.
No comments:
Post a Comment