Ndugu zangu,
Juzi usiku kwenye TBC1 iliripotiwa kuwa shilingi milioni mia mbili hazijulikani zilipo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Kamanda wa Takukuru mkoani Mbeya alionekana kwa uchungu kuzungumzia kashfa hiyo huku akiahidi kufanya uchunguzi na kuja na ripoti ndani ya kipindi kifupi. Kamanda huyo alisikitishwa na upotevu huo wa fedha za wananchi.
Kama shilingi milioni mia mbili zinapotea kwenye Halmashauri basi ina maana kuwa kuna ' panya' wanaotafuna fedha za wananchi kwenye halmashauri husika.
Kuna wenye kutakiwa kutolea ufafanuzi zilikokwenda fedha hizo. Wanajulikana. Na kwa vile imethibitisishwa kuwa kuna ' panya' wametafuna fedha za wananchi, basi, hao ni watuhumiwa uhalifu mpaka watakapothibitishwa vinginevyo.
Naam, vihenge ( Vya kuhifadhia mazao) vya WanaMbarali vimeingiliwa na panya. Chonde WanaMbarali, tukicheza na ' panya' waliovamia vihenge vyetu, tutaambulia pumba.
Tunasubiri hatua za vyombo vya dola zitakazofuata.
No comments:
Post a Comment