Wednesday, May 22, 2013

migori iringa, mapema asubuhi hii,MAANDALIZI UWEKAJI JIWE LA MSINGI.

jk f0ccf
Pilika pilika za maandalizi.

mgr1 a6624
 Uwekaji jiwe la msingi Barabara ya Iringa - Dododma, Hapa na kijiji cha Migori Mkoani Iringa.
mgr2 ccec3
Baadhi ya viongozi wakimsubiri mgeni rasmi
mgr f32d8
Muonekano wa sehemu ya Barabara hiyo.

Tuesday, May 21, 2013

Rais Obama kuzuru Afrika ikiwemo Tanzania


White House imesema Rais. Obama atakwenda Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.
White  House inasema rais wa Marekani Barack Obama atakwenda Afrika  mwishoni mwa mwezi wa sita ambapo atazuru nchi tatu.


Katika taarifa Jumatatu jioni, White House  ilisema rais Obama na mke wake Michelle watakwenda Senegal,  Afrika Kusini na Tanzania mwishoni mwa Juni na mapema mwezi Julai.
Utawala wa rais Obama  unasema rais huyu wa Marekani atakutana na maafisa wa serikali, viongozi wa kibiashara, asasi za kiraia na makundi ya vijana.

Safari ya bw.Obama itaanza Juni 26 mpaka Julai 3 na inalenga kudhihirisha mahusiano ya karibu kati ya Marekani na nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.

Rais Obama ambaye baba yake alizaliwa Kenya, alizuru Afrika  mara moja  katika muhula wake wa kwanza, alipotembelelea Ghana mwaka 2009.

Mkewe Michelle Obama pia amesafiri kwenda Afrika Kusini na Bostwana. Chanzo: voaswahili

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa



BonifaceWambura 95bcb

RCL KUUMANA RAUNDI YA PILI WIKIENDI

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao inaingia raundi ya pili wikiendi hii kwa kukutanisha timu 14 zilizofanikiwa kusonga mbele.


Timu zitakazocheza raundi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ni Abajalo ya Dar es Salaam itakayokuwa mwenyeji Kariakoo ya Lindi katika mechi itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Siku hiyo hiyo Uwanja wa Azam ulioko Chamazi utatumika kwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga wakati Jumapili (Mei 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Machava FC ya Kilimanjaro na Mpwapwa Stars ya Dodoma itakayochezwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Stand United ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida katika mechi itakayochezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Polisi Jamii ya Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana siku hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi. Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sabasaba.

Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu wakati timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI MECHI YA FIFA

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi (referee assessor) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Mechi hiyo ya Kundi B, Kanda ya Afrika kati ya Cape Verde na Equatorial Guinea itafanyika Juni 8 mwaka huu saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Verzea mjini Praia.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao watatoka Angola ni Martins De Carvalho Helder, Dos Santos Jerson Emiliano, Da Silva Lemos Julio na Muachihuissa Caxala Antonio. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Diarra Massa Momoye wa Mauritania.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Friday, May 3, 2013

JK AKUTANA NA WASHIKADAU WA SMART PARTNESHIP

 

sp2 a3b4a
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mkutano wa Smart Partnership leo Mei 3, 2013 Ikulu jijini
Dar es salaam.
sp3 5a1bb
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washikadau toka katika mashirika binafsi na ya umma
walioalikwa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mkutano wa Smart Partnership.