Wednesday, July 4, 2012

Serikali yakubali kujirekebisha mipaka ya mbuga ya Selous kuruhusu uchimbaji wa madini ya Urani.


SERIKALI kwa kushirikiana na kamati ya ulithi wa Dunia ya UNESCO imekubali ombi la kurekebisha mpaka wa pori la akiba la Selous ili kuruhusu uchimbaji wa madini ya Urani.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki alisema kamati hiyo katika kikao chake cha 36 kilichofanyika juni 24 mwaka huu Saint Petersburg nchini Russia imekubali ombi hilo.

Kagasheki alisema tayari kamati hiyo imetenga eneo la Km 200 kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo ambayo yataanzwaa kuchimbwa wakati wowote kuanzia sasa.

“Mimi nimerudi kutoka Russia ambapo nilikwenda kuhudhuria mkutano huo kwa niaba ya serikali, na kwa mara ya kwanza ombi hilo lilipelekwa kwa kamati hiyo ya urithi wa Dunia ya UNESCO mwezi julai 2011 ambapo lilijadiliwa katika kikao chake cha 35 na hatimaye limekubaliwa mwaka huu” alisema Kagasheki.

Alisema uamuzi huo ulifanyika ili kuruhusu tathimini ya ardhi mazingira na kukamilisha kwa kutoa muda kwa wataalamu kufika eneo linarohusika ili kuhakiki taarifa ya tathimini hiyo.

Wakati huohuo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wan chi za Kusini mwa Afrika utakaofanyika octoba 15 hadi 19 jijini Arusha mwaka huu ukiwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya utalii pamoja na uhifadhi katika hifadhi .

Aidha utajadili changamoto pamoja na mafanikio mbalimbali yakiwemo masuala ya ulinzi na usalama wa watalii na tanzania imechaguliwa kutokana na usalama wan chi ulioko hivi sasa na wageni wapatao 300 wanategemea kuhudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment