Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Tusamale Mwamlima amewataka watendaji wa serikali katika halmashauri ya Mji na wilaya ya Mpanda katika wilaya anayoongoza kumpatia ushirikiano wa karibu katika utendaji kazi katika utumishi wa umma ili kuwaletea wananchi maendeleo ambayo ndiyo wanayoyatengemea na kuachana mamalamiko kama watendaji wao.
Changamoto hiyo ameitoa leo wakati akiongea na watendaji wa halmashauri hizo alizitembelea ofisi ni kujitambulisha na kufahamiana tangu kuteuliwa na Mh.Rais Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa wilaya hiyo kufuatia aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyoDr Rajabu Rutengwe kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi.
Mkuu huyo wa wilaya almesema hakuna mtu yeyote anayefanikiwa bila kuwa na ushirikiano wa karibu bila ushirikiano hakuna mafanikio,hivyo anaomba ushirikiano wa karibu kwa watendaji na wananchi kwa ujumla.
Katika kikao hivyo mkuu huyo wa wilaya ametaja mambo matano yaliyoko mbele yao kwa ajili kuhakikisha yanatekelezwa ili kufanikisha maendeleo kwa wananchi ,moja ya mambo hayo ni uwepo amani ili kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika augost 26 mwaka huu,
Jambo la pili maazimisho ya sherehe za wakulima nanenane ambapo tunatakiwa kufanya vizuri ili kuweza kutunza ushindi uliopatikana mwaka wa jana katika maazimisho hayo ambapo wilaya ya mpanda iliibuka mshindi wa kwanza kikanda kwa kanda ya nyanda za ju kusini katika halmashauri za mikoa ya nyanda za juu kusini ambazo ni Mbeya, Rukwa, Ruvuma,Iringa,Katavi na Njombe.
Jambo lingine alilosisitiza kuhusu mbio za mwenge pamoja na maandalizi ya mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya,na kuwataka watu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha watu wanakuwa huru kutoa maoni yao kuhusu mchakato wa kuundwa kwa katiba mpya katika tume ya kukusanya maoni inayoongozwa na jaji Joseph walioba itakapotembelea mikoa kukusanya maoni watu wajitokeze kutoa maoni yao.
Kwa upandewake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilayaa ya Mpanda Justin Tibenderana alitoa taarifa fupi kwa mkuu huyo wa wilaya kwa kueleza hali ya wilaya na shughuli za maendeleo,hali ya kiutawala, na shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na shughuli za kilimo cha mazao ya biashara ambapo wanategemea zao la tumbaku na kahawa kwa kiasi kidogo,
Amesema kuwa kwa sasa wilaya imeazisha zao la kilimo cha miembe ili liwe zao la biashara ambalo litakuwa zao mbadala ya zao la tumbaku ambalo lianharibu mazingira.
No comments:
Post a Comment