WANAFUNZI wanane wa shule ya msingi,Pipaya iliyopo
wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha, wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji
wakati wakijaribu kuvuka mto wakati wakitokea shuleni wakielekea nyumbani
kwao.
Akidhibitisha kutokea kwa maafa hayo jana Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea
tarehe 27 mwezi huu majira ya saa 11.30 jioni katika kijiji cha Kiyaya Wilayani
Ngorongoro,mkoani Arusha.
Kamanda aliwataja marehemu hao kuwa ni Olonana
Mosirori(13)mwanafunzi wa darasa la saba,Nemao Faraji (14)mwanafunzi wa darasa
la tano,Lekinyani Eliakimu(11)mwanafunzi wa darasa la pili,Kisiyaya
Mbalinoto(13)mwanafunzi wa darasa la sita na Lapaine Lengukuwi(14)mwanafunzi wa
darasa la tano ambao miili yao ilipatikana.
Alisema kuwa tukio hilo lilitokea kufuatia mvua kubwa
iliyonyesha jana majira ya saa 9 alasiri wilayani humo na kusababisha maji kujaa
katika mito mbalimbali ,kiasi cha wakazi wakiwemo wanafunzi hao kushindwa
kuvuka.
Andengenye aliwataja wengine ambao miili yao bado haijapatikana kuwa ni Ponyangusi Mbalau(12)mwanafunzi wa darasa la tano,Logoi Oleiki(11)mwanafunzi wa darasa la pili.
Hata hivyo jeshi la Polisi Wilayani humo kwa
kushirikiana na Wananchi wanaendelea kutafuta miili mingine mitatu ambayo bado
haijulikani ilipo huku miili ya marehemu iliyopotikana ikikabidhiwa kwa ndugu na
jamaa kwaajili ya shughuli za mazishi.
Wakati huo huo Askari wa jeshi la wananchi
Tanzania(JWTZ), kikosi cha 977 Tanganyika Packers, Joseph Simsokwe (37)amekutwa
amekufa pembezoni mwa korongo ,baada ya kusomwa na maji ya mvua katika eneo la
Njiro kwa msola,nje kidogo ya jiji la Arusha.
Kamanda Andengenye alisema kuwa tukio hilo la kukutwa
kwa mwili hulo,lilitokea juzi majira ya saa 3 asubuhi ambapo polisi waliokuwa
doria waliukuta mwili huo ukiwa umekwama kwenye korongo.
Alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia askari polisi walifika na walipouchunguza mwili huo walibaini kuwa marehemu alikuwa ni askari wa JWTZ na alikutwa na jeraha kubwa la mshono katika mguu wake wa kulia linalodaiwa kutokana na ajali ya pikipiki.
Kwa mujibu wa majirani na marehemu huyo wamedai ya kuwa
mwanajeshi huyo alikuwa akitumia pombe nyingi kupita kiasi na kwamba siku ya
tukio anadaiwa kuwa tayari alikuwa amekunywa pombe hali iliyosababisha ashindwe
kumudu kuvuka mto na kusombwa na maji yaliyosababisha kifo chake.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospital ya mkoa Mount Meru,kwa ajili ya uchunguzi zaidi
,polisi bado wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo.
Katika tukio jingine,mwanafunzi wa kidato cha pili
katika shule ya sekondari ya Arusha day,mkazi wa Olmatejoo,Emanuel
Agrey(15)amejinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake mzazi hadi kufa kwenye
kamba ya kuanikia nguo.
Kamanda Andengenye alifafanua kuwa tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 10 jioni katika eneo la Olmatejoo ,ambapo mama mazazi wa
marehemu huyo,Magreth Stewart (37) aliukuta mwili wa mtoto wake ukiwa
umening’inia kwenye kamba hiyo ya kuwanikia nguo alipokuwa akitoka
kanisani.
Alisema kuwa mama huyo baada ya kuona mwili huo alitoa
taarifa kwa watu mbalimbali akiwemo mume wake,Agrey Stewart ambapo kwa pamoja
waliingia ndani na kushuhudia tukio hilo na baadae walitooa taarifa kituo cha
polisi ,ambao askari polisi walifika na kuondoka na mwili huo.
Kwa mujibu wa kamanda Andengenye chanzo cha tukio hilo
bado hakijajulikana na kwamba polisi wanachunguza tukio hilo huku na mwili wa
mwanafunzi huyo ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya
mkoa mount Meru.
No comments:
Post a Comment