Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic
Kacou (kulia) akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani Bw. John Hendra (katikati). kushoto ni
Country Representative UN Women Bi. Anna Collins-Falk.
Bw. Kacou amezungumzia tamko lilitolewa na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa la kutaka Dunia kuungana kwa pamoja katika kukomesha
ukiukwaji wa haki za Wanawake Duniani.
Aidha Bw. Kacou ametoa shukrani za dhati kwa Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa kuonyesha nia ya
dhati katika kupiga vita unyanyasaji wa Wanawake ambapo amesema kwa kuonyesha
mfano Rais huyo amewapa nafasi za uongozi na kusema kuwa Wanawake wakiwezeshwa
wanaweza.
Umoja wa Mataifa kwa kupitia Shirika lake la wanawake
leo umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani kwa kutoa wito kwa jamii
kushirikiana kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es
Salaam leo, Assistant Secretary-General, Deputy Executive Director for Policy
and Programme wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa John Hendra amesema
Umoja wa Mataifa unaunga mkono juhudi za Tanzania katika kukabiliana na
ukiukwaji wa haki za mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla.
Awali akimkaribisha Bw. Hendra, Mwakilishi Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou amesema Umoja wa Mataifa
unafanya kazi bega kwa began a serikali ya Tanzania katika kufanikisha
utekelezaji wa sera ya haki na usawa kwa wanawake na wanaume.
No comments:
Post a Comment