Utangulizi
Nimesoma katika gazeti la Habari Leo la Alhamisi,tarehe
8/3/2012 toleo namba 01901,lenye kichwa cha habari “Askofu Kutanzua Lugoba
Jumapili”.Kabla ya hapo nilizisikia hizi habari kutoka kwa ndugu zangu hitakuwa
si vyema kama sitatoa maoni yangu juu ya hili kwa jamii.
Ninavyomfahamu Pd.Mkude.
Nilimfahamu Pd.Mkude mwishoni mwa miaka ya 80 wakati
nikiwa nasoma Morogoro Sekondari.Gazeti nililonukuu liemwandika kama Pd.Phillipo
Mkude,lakini sisi tulimfahamu kama Pd.Phillip-Neri Mkude.Wakati huo akiwa
Headmaster wa Kigurunyembe Sekondari.Alitoa mchango mkubwa sana katika
taaluma,nidhamu na michezo.Itakumbukwa kuwa yeye ndiye alijenga uzio ili
kudhibiti utoro ambao ulikuwa umekithiri.Kitaaluma sitaongea kwani hatuwezi
kumaliza,isipokuwa katika michezo amefunda nguli wengi katika uchezaji mpaka
uongozi wa kitaifa.Mfano ni aliyewahi kuwa katibu mkuu wa FAT,Michael Wambura na
nduguye ambaye ni msemaji wa TFF,Boniphace Mgoyo Wambura ambaye wakati ule
alikuwa mkoba mahili sana.Kadhalika hatuwezi kusahau wachezaji mahili kama akina
David Joseph Mihambo ambaye aliwika na wekundu wa Msimbazi na timu ya
Taifa.
Haikuwa ajabu kumuona kasisi huyu akisimama kama kocha
kuhamasisha vijana wake akiwa amevalia shati la kichungaji.Hakuishia
hapo,ilikuwa ni kawaida yake kuandamana na vijana wake hata katika
mijadala(debate)wakati ule.Ilipendeza sana na alifurahisha wengi.Kwa
ziada,nifahamuvyo mimi huyu si ndugu na Askofu Mkude wa Morogoro na huenda hata
koo zao zisifanane kwa desturi ya kabila hili lilivyo.
Madai Juu Ya Pd.Mkude.
Katika gazeti la habari leo Pd.Mkude anadaiwa kuwaita
Wakwere ni wachafu,masikini,hawasomi na wanaendekeza kucheza ngoma.Amenukuliwa
na majibu yake lakini mimi siyahitaji kwa kuwa ninaangalia kauli anazotuhumiwa
na kutoa maoni yangu,kwani nayaelewa kiasi mazingira ya Ukwere.Mimi ni Mkwere na
mama yangu ni mluguru,kabila atokalo Pd.Mkude.(I declare my
interests).
Pd.Mkude ni jasiri na anafaa kuwa kiongozi.Ni viongozi
wachache sana wa kijamii,kiroho na hata kisiasa wenye uwezo wa kuwaambia watu
udhaifu wao.Ndio maana tunaendelea kutafunwa na uzinzi,maradhi,ufisadi na
mengineyo.Maneno aliyoyasema kasisi huyu juu ya Wakwere ni kweli na wala hana
sababu ya kuwadhalilisha;ili apate nini?Angalia leo hii Wakwere wauzavyo maeneo
ya barabarani kwa bei ya kutupa,sasa huu si umasikini? Tembelea vijiji vingi
Tanzania hii wenyeji wanavyochangamkia nyumba za matofali ya kuchoma;ukwele wao
kimya.Sasa mtu wa namna hii atajenga choo bora? Kuhusu shule nalo kweli
mnahitaji mjadala?Ni nani asiyejua kuwa kuna baadhi ya mikoa ukitangaza nafasa
ya kazi utapata zaidi ya aslimia 90 ya wenye sifa ni wenyeji asilia,kwa Ukwere
nadhani hata utangaze kijijini waweza pata si zaidi ya aslimia 25,sasa hili nalo
uongo ni upi? Tembelea mashule,vyuo utapata ukweli,sasa tunabisha
nini?
Mbinu shindanishi(Maneno yangu si rasmi)
Pd.Mkude ametumia mbinu ambayo inawaumiza Wakwere na
kuwafanya waamke na kujua walipo na kuchukua hatua.Mbinu hii hutumiwa hata na
wazazi wanapokuwa na mtoto ambaye ni mvivu wa kula humwambia kuwa wewe hata
fulani anakushinda,ili apate uchungu na asikubali kushindwa,kasha amalize
chakula.
Nahisi kasisi huyu hakueleweka na jamii husika au kuna
kundi la wachache ambao si wenyeji asilia au wanatumia udhaifu wa wenyeji
kumfanya kasisi huyu aonekane mbaya.Kwa kuwa wanajua wenyeji wakiamka hawatapata
mashamba na viwanja kwa bei ya chee,pia wenyeji wakisoma watampa nani soda na
maji akimbizane nazo katika mabasi? Kwa kweli inasikitisha sana!
Kuhusu ngoma,Mluguru na Mkwere hawana tofauti hata huko
kwao Tangeni wanacheza,isipokuwa lazima tuwe na vipau mbele.Nina imani
alimaanisha hivi na si vinginevyo.
Maoni Yangu
Naamini wanaomtuhumu Pd.Mkude hawana nia njea na
Wakwere.Nahisi si wenyeji asilia au wanatumiwa bila kujijua kupiga vita mtu
yeyote anayetaka kuamsha mawazo ya wenyeji.
Hitimisho
Ndugu zangu,tulime,tusomeshe watoto wetu,tusiuze ovyo
ardhi zetu.Kama mtu anataka ajenge mkatane baada ya muda fulani inarudi
kwako.Tutakuwa wageni wa nani?
Mwandishi,Clarence F.Mahunda,anapatikana kwa simu 0713
722 398 na barua pepe:c.mahunda@yaoo.com
No comments:
Post a Comment