Wanafunzi washule mbalimbali zilipo katika Halmashauri ya Mji Mpanda wakishiriki maandamo ya sikukuu ya wanawake Mjini mpanda kuelekea sehemu ambako sherehe hizo zilizofanyika katika uwanja wa Kashaulili mjini hapa
Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari mjini mpanda wakiwa wamebeba mapango katika siku ya wanawake duniani yaliyofanyika jana 8/03/2012
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengwe akikagua vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza katika sherehe hiyo ya wanawake duniani katika uwanja wa Kashaulili
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengwe akipokea maandamano katika uwanja wa kashaulili mjini mpanda katika sikukuu ya wanawake ambapo kiwilaya yalifanyika katika kata ya sitalike
Mwl Asha Selemani wa shule ya Msingi Katavi akisoma lisala kwa mgeni rasmi katika sherehe ya wanawake duniani mjini hapa kwa niaba ya wanawake wenzake waliohudhuria sherehe hizo katika uwanja wa kashaulili
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengwe akiwahutubia wananchi walifika katika maadhimisho ya sikukuu ya wanawake Duniani iliyofanyika katika uwanja wa kashaulili mjini mpanda zaidi akisisitiza juu ya elimu na kuwaomba wazazi wawapatie elimu watoto wao wa kike kwani mwanamke akiwezeshwa anaweza na akakemea vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu hususani kile kuwabigana kuwabaka watoto wa kike kwa wanaume
Wanafunzi mbalimbali wa shule za sekondari mjini hapa wakisakata musiki(lumba)katika uwanja wa kashaulili katika sikukuu ya wanawake katika uwanja huo
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengwe akikagua mirada ya wanawake katika sherehe za wanawake duniani katika viwanja vya kashaulili mjini hapa
Mkuu wa wilaya ya Mpanda akitoa zawadi kwa watoto yatima wa Halmashauri ya mji Mpanda katika uwanja wa kashaulili mjini hapa
No comments:
Post a Comment