Ofisa Ustawi Jamii Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro,
Tabitha Majiku (kulia) akitoa neneo la shukrani baada ya kupokea msaada wa
fedha za kusaidia miradi ya maji mkoani humo kutoka Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Rufaa Mkoa
wa Morogoro. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve
Kilindo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk. Ntobi
Mwakibete (wa pili kulia).
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria
wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto) akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh. milioni 24.9 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa
Mkoa wa Morogoro, Dk. Ntobi Mwakibete za kusaidia kuchimba kisima cha maji.
Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
No comments:
Post a Comment