Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Somalia ambayo imekua ikijaribu
kujikwamua toka vita vya miaka 20 imetuma maombi yakutaka kujiunga na Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya
hiyo imethibitisha kupokea maombi ya Somalia.
Somalia inakuwa nchi ya tatu baada ya Sudan
Kusini na Sudan Khartoum kutuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya hiyo ya
Afrika Mashariki.
Hata hivyo azma ya Sudan kutaka kujiunga na
jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki imekataliwa.
Kwa sasa jumuiya ya Afrika Mashariki
inajumuisha nchi tano, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.
Mbali na nchi wanachama kuwa na ruhusa ya
kufanya biashara bila vikwazo vyovote kwa wakati huu zinapanga kuwa na sarafu
moja kufikia mwaka mwezi Juni mwaka huu wa 2012
Source:BBC
No comments:
Post a Comment