TAARIFA KWA UMMA
UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe
10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT),
tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
... 1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine
anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya
kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi
(Machine).
2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa
kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona
kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha
yake.
3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa
kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa
yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.
4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni
kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi
mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa
ziwepo mahospitalini zinakohitajika.
5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu
tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.
TAMKO LETU:
JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA
ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA
NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.
KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA
WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI
MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.
PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA
KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY
NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY
NKYA.
MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI
MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA
UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA
KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.
SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)
No comments:
Post a Comment