Pichani Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi.
Maimuna Tarishi akitoa taarifa ya kifo cha Elias Mzee ofisa mkuu wa
idara ya wanyamapori na mkuu wa kikosi cha kudhibiti ujangili kanda ya
Arusha, ambaye amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni katika
manispaa ya mji wa Iringa. Picha: Oliver Motto
Maimuna Tarishi akitoa taarifa ya kifo cha Elias Mzee ofisa mkuu wa
idara ya wanyamapori na mkuu wa kikosi cha kudhibiti ujangili kanda ya
Arusha, ambaye amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni katika
manispaa ya mji wa Iringa. Picha: Oliver Motto
Ofisa wa Idara ya wanyamapori amekutwa akiwa amekufa ndani ya chumba
chake , katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo ndani ya manispaa
ya mji wa Iringa, wakati akijipumzisha kusubiri mkutano mkuu.
Ofisa huyo aliyefahamika kwa jina la Elias Mzee ambaye ni mkuu wa
kikosi cha kudhibiti ujangili na ofisa wanyamapori mkuu kanda ya
Arusha, ambaye alikuja mkoani hapa kwa lengo la kuhudhuria mkutano
mkuu wa watendaji wa wizara na taasisi za Maliasiri na Utalii. Hayo yamebainishwa katika hotuba ya mkutano huo, wakati katibu mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi, akitoa taarifa
hiyo kwa watendaji wakuu wa wizara ya Utalii, mbele ya Waziri wa
Maliasiri na Utalii, mh. Ezekiely maige.
Bi. Tarishi amesema, Ofisa huyo, Elias Mzee amemkutwa na mauti usiku
katika nyumba ya kulala wageni, marehemu alipokuwa amekwenda
kujipumzisha, akisubiri mkutano mkuu huo, ambao mgeni rasmi alikuwa
Waziri wa Maliasiri na Utalii, Mh. Ezekiely Maige.
Naye Waziri Maige ametoa salamu za pole kwa watumishi wa Wizara hiyo
na idara ya Wanyamapori, huku mkutano ukikaa kimya kwa dakika moja,
hiyo ikiwa ni ishara ya kumkumbuka mtumishi mwenzao.
Mkutano huo, wenye lengo la kuboresha na kuimarisha Sekta ya Maliasiri
na Utalii , umefanyika katika ukumbi wa Veta mjini Iringa, huku
ukihudhuliwa na watendaji wakuu wa Wizara na taasisi ya maliasiri na
Utalii kutoka mikoa yote nchini.
No comments:
Post a Comment