ZAIDI ya shilingi Bilioni 140 zinapotea kupitia ukusanyaji wa mapato
katika Wizara ya Maliasili na Utalii, kila mwaka.
Akitoa taafa hiyo katika mkutano wa watendaji wakuu wa wizara na
taasisi za Maliasili na Utalii, Waziri wa Wizara ya Maliasiri na
Utalii, Mh. Ezekiely Maige amesema sekta hiyo inapoteza mapato hayo
kila mwaka kutokana na zao la Nyuki na Asali, kutopewa msukumu wa
kutosha.
Maige amesema jumla ya shilingi Bilioni 200 ambazo zinatakiwa
kukusanywa kwa mwaka, Wizara imekuwa ikipata shilingi Bilioni 60
pekee, na hivyo kuwepo kwa upungufu wa shilingi Bilioni 140.
Amewaagiza watendaji wa taasisi na Wizara hiyo kuimarisha usimamizi
katika ukusanyaji wa wa maduhuli ili fedha zote zinazopaswa kupatikana
zikusanywe, ikiwa pamoja na kuwahimiza wataalamu hao kuongeza
uzalishaji wa miti kwa kuzingatia mahitaji ya Mbao.
Aidha amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo, Wizara imejipanga
kuogeza uzalishaji wa asali, kupitia ufugaji wa Nyuki, ikiwa pamoja na
kutafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi, kwa lengo la
kudhibiti upotevu wa fedha hizo.
No comments:
Post a Comment