TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Ludewa
imemfikisha Mahakamani mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo
Mathei Kongo kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa.
Kufikishwa mahakamani kwa Kongo kumekuja siku moja tu baada ya
kukamatwa na taasisi hiyo machi 12 mwaka huu katika bar na hotel moja
wilayani humu alikokutwa akila chakula cha jioni.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Mohamed Siriti hakimu wa mahakama ya
wilaya ya Ludewa, mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa Lestituta Kessy amesema mshtakiwa
alitenda kosa hilo kati ya desemba mwaka jana na machi mwaka huu.
Kessy ameiambia mahakama kuwa kwa nyakati tofauti mshtakiwa aliomba
kupewa fedha jumla ya shilingi Milioni 1 na shilingi milioni 3 ili aweze
kumsaidia kupata zabuni samson Mwaipugile ikiwemo kusambaza computa
katika taasisi mbalimbali wilayani humo.
Mwendesha mashtaka Katika kosa la kwanza chini ya kifungu cha 15(1)(a)
cha taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ameiambia mahakama kuwa
kati ya disemba na machi mwaka huu aliomba fedha hiyo na machi 12
mwaka huu alipokea shilingi laki moja kupitia kwa wakala wake.
Hata hivyo mshtakiwa huyo Mathei Kongo ambaye ni mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Ludewa mbele ya mahakama amekana kuhusika na
makosa yote yanayomkabili.
No comments:
Post a Comment