Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama
mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo mjini Moshi jioni hii.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete
wakipokewa kwa furaha walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) jioni hiitayari kwa ziara ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara
alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hii. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi
jioni ya leo, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Miongoni mwa
shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya
kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa
kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro
Speak Out, Climb Up”.
Shughuli hiyo
itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali na
kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa
Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini
Moshi.
Hii ni ziara ya
kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa
huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment