Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mpanda Mhe;
Enock Gwambasa
akifungua kikao cha walimu wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengwe akiwapongeza walimu kwa kufaurisha wanafunzi na kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo
Kaimu Mkurungezi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Bw. Abdallah Kinelo akijibu kero na ombi la kutengewa viwanja kwa walimu
Afisa Elimu wa shule za Msingi katika Halmashauri ya Mji Mpanda Bi Irine Makungu akiwa akijibu baazi ya maswali yaliyoulizwa na walimu
Afisa rasilimali watu wa Halmashauri ya Mji Bw. Mwinyikombo akijibu maswali yaliyoulizwa na walimu katika idara ya fedha na kupandishwa kwa madaja ya walimu
Afisa Elimu Sekondari Bw. Mwapongo akijibu maswali yaliyoulizwa na walimu na kutoa maelezo juu ya usafiri wa gari la shle ya wasichana Mpanda Girl's na kusema kuwa atatoa gari la zalula kwa ajili ya shule kwa matatizo yatakayotoke usiku
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengwe akimpongeza Afisa Rasilimali watu Bw. Mwinyikombo kwa kujibu kero mbali mbali za walimu katika Halmashauri yake ya Mji na kuahidiwa tai ya shingoni yenye bendera ya Taifa na mkuu wa wilaya
Hawa ni baazi ya walimu waliohudhuria kwenye kikao cha walimu kilichofanyika jana tarehe 03/03/2012 katika ukumbi wa St Mary's Mpanda
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mpanda Mh: ENOCK GWAMBASA
ameitisha kikao mwishoni mwa wiki hii ili kubadilishana mawazo na walimu wa
halmashauri yake, vievile waliweza
kuhudhuria wakuu wa idara mbalimbali na
wasaidizi;
Mgeni rasmi wa kikao hicho alikuwa DKT RAJABU RUTENGWE ambae
ni mkuu wa wilaya na mkoa mtarajiwa wa katavi
Mwenyekiti wa Halmashauri alieleza mafanikio,changamoto na mipango mbalimbali inayoikabili Halmashauri ya mji wa mpanda ikiwemo ujenzi wa chuo kikuu cha kisasa cha kilimo kiitwacho katavi Agricuture university
Walimu waliweza kuuliza maswali mbalimbali ikiwemo kutokupatikana
kwa salary slip ya mwezi wa nane mwaka 2008 hazijapatikana hivyo
inawasababishia usumbufu wakati wa kustafu
Na waliomba kupewa maeneo ya kujenga nyumba kwa bei nafuu
kitu ambacho kitasaidia walimu wa
Halmashauri ya mji mpanda kutohama katika Halmashauri yao
Mwenyekiti wa Halmashauri aliwapongeza walimu kwa kufaulisha wanafunzi wa shule ya msingi na kuwa wa kwanza kimkoa kwa miaka mitatu mfululizo
Baada ya hayo yote mkuu wa wilaya aliitimisha kwa kuwapongeza walimu kwa jitihada
mbalimbali wanazozifanya katika kusukuma gurudumu la maendeleo na alisisitiza swala la
mawasiano ndio nguzo kuu katika utumishi
No comments:
Post a Comment