Friday, March 2, 2012

BARAZA LA MITIHANI LAWAPA MAFUNZO WALIMU 76

Baraza la mitihani la Taifa lawapa mafunzo walimu 76 Wilaya ya  Mpanda vijijini juu ya uendeshaji wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa kutumia teknolojia ya OMR, 2012 (Optical Marck Reader) jana wilayani hapa
Kaimu Mkurugenzi Mama N.Nkoo ambaye pia ni 
Afisa Elimu Wilaya akifungua mafunzo hayo 

Bwana Joshua Sanga Mwakilishi wa baraza la Mitihani akitoa mafunzo 
elekezi kwa washiriki wa mafunzo ya OMR Wilayani Mpanda 

Baadhi ya wawakilishi kwenye mafunzo ya OMR wakimsikiliza mmoja kati ya  watoa 
mada kwa makini kataka mafunzo hayo

 Mafunzo haya yalifunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Mama N.Nkoo ambaye pia ni Afisa Elimu wa Wilaya hii. Mada mbalimbali zilijadiliwa kuhakikisha walimu waliohudhuria mafunzo hayo wanaelewa vema na kufanya mazoezi ya kutosha ili waweze kuwaelekeza walimu wengine katika kata zao

Mada hizo ziliendeshwa na Afisa Elimu Taaluma Bwana Filbert Nguvumali, Afisa Elimu Vielelezo na Takwimu Bwana Lebai Swallo na mwakilishi toka Baraza la mitihani Bwana Joshua Sanga

Mada zilizojadiliwa  ni pamoja na mabadiliko ya uendeshaji wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi PSSE, 2012. Taratibu za kutumia fomu maalumu za kujibia mtihani , ujazaji fomu maalum za kujibia mtihani, Utaratibu wa usajili wa watahiniwa wa kumaliza elimu ya msingi  PSSE, 2012, Uandaaji wa ripoti mbalimbali na kufanya mazoezi kwa kutumia fomu ya OMR

Walimu hao wakiwa ndiyo wawakilishi wa walimu wengine waliobaki shuleni zaidi ya 1000 walipokea kwa furaha mafunzo hayo na kukili watajitahidi kwa nguvu na mali kuwasilisha ujuzi huo kwa walimu wengine.

No comments:

Post a Comment