Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga
akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa Halmashauri za Serikali
za Mitaa na Sekretarieti za mikoa jana jijini Dar es salaam . Mkutano huo
uliwajumuisha wakaguzi 165 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara kwa lengo la
kuwaelimisha juu ya miongozo ya ukaguzi wa ndani imetolewa hivi karibuni ili
kuboresha ukuguzi wa ndani utakaoleta matokeo mazuri ya rasilimali na fedha za
wananchi .
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga
ameagiza wakaguzi wote wa ndani kuhakikisha kuwa wanasimamia rasilimali za nchi
vizuri kwa niaba ya wananchi ili miradi ilinganishe na thamani ya
fedha iliyoombewa.
Mtonga alitoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa
siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa Halmashauri za Serikali za Mitaa na
Sekretarieti za mikoa jana jijini Dar es salaam .
Alisema inasikitisha kuona ubadhirifu wa mali za
Serikali kama vile ujenzi wa madarasa hayakidhi viwango unatokea mita chache
toka Ofisi kwa Mkaguzi wa Ndani au mtaa anaoishi bila kuchukua
hatua zinazostahili za kuhakiki kama kweli mradi huo unalingana na fedha
zilizotolewa na Serikali.
Mtonga aliwaagiza wakaguzi wa ndani kuwa wabunifu ili
wawe wasimamizi wazuri wa rasilimali na fedha umma kwa niaba ya wananchi bila
kujali kuwa wanavifaa vya kutosha au hawana .
Aidha Mkaguzi Mkuu huyo wa Ndani wa Serikali aliwaonya
Wakaguz hao kuepuka tabia ya Ushirikiano na mitandao inayowafanya kikiuka sheria
na taratibu za fedha ambazo ndio zinaweza kusababisha kutoa taarifa zisizokuwa
za sahihi za ukaguzi wa ndani na hivyo kusababisha upotevu wa fedha za
umma.
Alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa inatokea tukio
kama la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambalo lilitokana na
ukaguzi maalumu wa mwaka 2007/2008 hadi 2009/2010 wakati Mkaguzi wa Ndani yupo
.
Katika hatua nyingine Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali
Mtonga alisema kuwa Ofisi yake inaandaa Mwongozo utakaowasaidia wakaguzi wa
Ndani kukaguzi bajeti na kuangalia utekelezaji wake.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kunakuwepo kwa uwazi na
uwajibikaji kwa watendaji ili mwananchi ajue bajeti inakwendaji na kitu gani
kinatakiwa kufanyika ili kumletea maendeleo kulingana na mapendekezo ya
vipaumbele vilivyoombewa fedha.
No comments:
Post a Comment