Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Mamlaka ya ziwa
Tanganyika umefanyika leo mkoani
Kigoma, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba
uliounda mamlaka hiyo.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira) Dk.
Terezya Huvisa amesema kuwa ili kulinusuru Ziwa
Tanganyika jitahada za Nchi zote nne ni
muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazolikabili
ziwa hilo kwa sasa kwa kutumia
fursa zilizopo.
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na uchafuzi
mkubwa wa mazingira ikiwa ni
pamoja na kujaa kwa taka za majumbani na zile za
viwandani, uvuvi haramu kutokana
na ongezeko la watu, kilimo na ufugaji usio endelevu.
Hata hivyo Waziri Huvisa
amewakumbusha wajumbe wa Mkutano huo kuwa Ziwa
Tanganyika linaunganisha Nchi zote
nne badala ya kuzitenganisha, hivyo ni muhimu kuwa na
mikakati endelevu ya kuhifadhi ziwa
Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano huo
ni pamoja na Utekelezaji wa
Mpango Mkakati wa Kitaifa ambao kwa sasa unafanya kazi
katika nchi zote pamoja na
Mkakati wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuwa na
usimamizi endelevu wa Ziwa Tanganyika
baadaya ya mwaka 2013 ambapo fedha za wafadhili
zitafikia kikomo.
Katika Mkakati huo wa kukusanya fedha Nchi zote nne
zimetia saini makubaliano ya
kuchangia fedha ili hifadhi ya Ziwa hilo iwe endelevu,
ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa
miradi mbalimbali.
Mkutano huo umefanyika Tanzania kwa mara ya pili,
mkutano mwingine kama huo ulifanyika
jijini Dar es Salaam mwaka 2007. Mamlaka hiyo ya Ziwa
Tanganyika inaundwa na nchi za
Zambia, Burundi, Congo (DRC) na mwenyeji
Tanzania.
No comments:
Post a Comment