WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
S.L.P 70069, DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho
Kikwete amevialika vyama vya siasa vyenye usajili wa
kudumu, jumuiya za
kidini, asasi za kiraia na makundi mengine ya watu
wenye malengo yanayofanana
kuwasilisha kwake orodha ya majina ya watu
watakaoteuliwa kuwa Wajumbe wa
Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu
Mabadiliko ya Katiba.
Mheshimiwa Rais ametoa mwaliko huo kupitia Tangazo la
Serikali Na. 66 la tarehe
24 Februari, 2012 kwa mamlaka aliyopewa chini ya
kifungu cha 6(6) cha Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.
Kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
2011 kinamtaka Mheshimiwa
Rais kualika vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu,
jumuiya za dini, asasi za
kiraia, jumuiya, taasisi na makundi mengine ya watu
wenye malengo yanayofanana
kuwsilisha kwa Rais orodha ya majina ya watu kwa ajili
ya kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume.
Kwa mujibu wa Tangazo hilo la Serikali, kila chama cha
siasa chenye usajili wa
kudumu, jumuiya ya kidini, asasi ya kiraia na kila
kundi lenye watu wenye malengo
yanayofanana itapaswa kuwasilisha orodha ya majina
yasiyozidi matatu ambayo
itaonyesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali
anapoishi kila mtu aliyemo katika
orodha.
Aidha, orodha hiyo inatakiwa iwasilishwe kwa Mheshimiwa
Rais kwa maandishi
ama moja kwa moja kwa mkono au kwa rejista ya posta
kupitia anuani ifuatayo:
i.
ii.
Ama: Katibu Mkuu Kiongozi,
Ikulu,
S.L.P. 9120,
DAR ES SALAAM
Au:
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu
Kiongozi,
Ofisi ya Rais,
S.L.P. 4224,
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment