
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akiweka jiwe la msingi
katika Kituo Kikuu cha Afya Tarafa ya Inyonga Leo. Kituo hicho
kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 64 pamoja na nyumba za
watumishi 24.
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mpanda Injinia Emmanuel Kalobelo akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Mhe.
Makamu wa Rais. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia
Stella Manyanya na kushoto kwake ni Mke wake Mama Asha Billal na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Rukwa Mhe. Hiporatus Matete.
Makamu wa Rais akikagua
jengo la kituo hicho
AKIWA ZIARANI MKOANI RUKWA MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MTAFITI BIGWA WA SOKWE DUNIANI AMBAYE PIA NI MTAALAMU WA MAZINGIRA IKULU NDOGO YA MPANDA
Si mwingine bali ni Jane
Goodall ambaye ana zaidi ya miaka 73 mwanamama mtafifiti bigwa wa masokwe
duniani kutoka Uingereza ambaye pia ni mtaalamu wa mazingira kwa pamoja Mhe.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal anayeonyesha kitabu cha mwanamama
huyo kiitwacho "Reason for Hope" kwa baadhi ya waandishi wa habari waliojumuika
nao kwenye chakula cha jioni Ikulu ndogo ya Mpanda jana. Mama Jane ametumia
zaidi ya miaka 40 ya utafiti wake katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyopo
Mkoani Kigoma akitafiti maisha na tabia za Sokwe wanaopatikana kwa wingi katika
mbuga hiyo.
.
Mtafiti Jane Goodall
akimuonyesha Mhe. makamu wa Rais moja ya tabia za nyani ambayo ni salamu
inayotumiwa na mnyama huyo ambaye hushika kichwa kama ishara ya maamkizi. Jane
Goodal pia ni balozi wa mazingira na viumbe hai duniani katika kuhamasisha
umuhimu wa uhai wa vitu hivyo pamoja na ustawi misitu.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt.
Mohammed Gharib Bllal akishika mdoli wa nyani ambao unamilikiwa na Mama Jane
Goodgall kwa takribani miaka 15 sasa. Alisema kuwa anamiliki mdoli huo kutokana
na hisia zake juu ya nyani ambao amekuwa akiwatafiti katika kipindi chote cha
maisha yake.
Mama Asha Billal Mke wa Makam
wa Rais na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakiwa wameshikilia mdoli huo ambao kwa hakika
anavutia pamoja na historia yake.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt.
Rajab Rutengwe naye hakuwa nyuma kwani alimtia mkononi mdoli huyo wa
kihistoria.
Mama Jane Goodall
akikumbatiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kabla ya kuondoka
katika Ikulu hiyo ndogo ya Mpanda jana usiku.
Picha ya pamoja kati
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal na Mama Jane Goodal. Kulia kwa Makamu
wa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, wa pili anayefuata na
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima. Kushoto kwa Mama Jane
Goodall ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda
Dkt. Rajab Rutengwe.
TAAARIFA YA MKOA WA RUKWA ILIYOSOMWA NA MKUU WA MKOA HUO KWA MAKAMU RAIS AMBAYE YUPO MKOANI HUMO KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU SABA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akisoma taarifa yake ya Mkoa kwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Billal katika ukumbi wa
Ikulu Ndogo ya Mpanda mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kikazi ya
siku saba Mkoani Rukwa.
Mhe. Makamu wa Rais
akifuatilia hotuba hiyo mstari baada ya mstari katika ikulu ndogo mjini mpanda
TAARIFA
YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MHE.
DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL
KATIKA
ZIARA YAKE MKOANI RUKWA
TAREHE
18 - 24 FEBRUARI, 2012.
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
1.0.
UTANGULIZI.
Mheshimiwa Makamu wa Rais,
Awali ya yote
napenda kuchukuwa fursa hii kukukaribisha wewe na ujumbe wako hapa Mkoani Rukwa.
Sisi wananchi wa Mkoa wa Rukwa tunafarijika sana pindi tunapotembelewa na viongozi wa
Kitaifa kwani tunajua wazi tutapata ushauri, maelekezo na maagizo kwa ajili ya
kuboresha utendaji wetu wa kazi.
Mheshimiwa Makamu wa Rais,
Taarifa hii
inazungumzia habari za Mkoa wa Rukwa ambao ni pamoja na Mkoa mpya wa Katavi.
Inaonyesha ulipo mkoa na umbile lake . Aidha, tunaelezea mafanikio na changamoto
zilizomo katika sekta mbalimbali ikiwemo
Elimu, Afya, maji, Kilimo, Ushirika, Uvuvi, Ardhi, Maendeleo ya jamii, Biashara,
Viwanda, Miundombinu, Mawasiliano na Masuala mtambuka. Pia hatukusahau
masuala ya Haki za Binadamu na Utawala bora.
MAKAMU WA RAIS AWASILI WILAYANI MPANDA LEO KWA ZIARA YA SIKU 7 MKOANI RUKWA
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya mara baada ya kuwasili katika uwanja
wa ndege wa Mpanda leo kwa ziara ya kikazi ya siku saba Mkoani
Rukwa.
Mhe. Makamu wa Rais
akisalimiana na wananchi wa Mpanda mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa
Mpanda tarayi kwa kuanza ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa. Anayeongozana
naye kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya. Makamu wa
Rais anategemea kufanya ziara yake katika wilaya zote tatu za Mkoa wa Rukwa
ikiwepo Mpanda yenyewe, Nkasi na Mpanda ambapo atahitimisha ziara hiyo tarehe 24
Februari na kuelekea Mkoa jirani wa Mbeya
Makamu wa Rais Dkt.
Mohammed Gharib Billal akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
leo kwenye uwanja wa kashaulili wilayani Mpanda. Miongoni mwa mambo
aliyosisitizia katika mkutano huo ni pamoja ujenzi wa mabweni katika shule za
Sekondari kwa ajili ya wasichana kusaidia kuwaepusha na mimba za mashuleni.
Aidha alisisitiza kuhusu upandaji miti kuepukana na athari za mabadiliko ya
tabia nchi.
MAKAMU WA RAIS KUFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 7 MKOANI RUKWA
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Gharib
Billal.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Mohammed Gharib Billal atafanya ziara ya siku saba Mkoani Rukwa ambapo
itajumuisha pia Mkoa mpya wa Katavi. Ziara yake hiyo itaanza tarehe 18 na
kumalizika tarehe 24 Februari 2012 akitokea mkoani Ruvuma.
Awapo Mkoani Rukwa atatembelea
Wilaya zote tatu za Mpanda, Nkasi na Sumbawanga. Mpanda atakuwepo kuanzia tarehe
17 hadi tarehe 20 ambapo atapokea taarifa ya Serikali pamoja na Chama cha
Mapinduzi. Aidha atafanya mkutano wa ndani katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Mpanda
na mikutano wa nje katika uwanja wa Kashaulili na Ofisi ya Tarafa
Inyonga.
Pamoja na hayo atapata fursa
ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya katika tarafa ya Inyonga na
kufanya Mkutano wa hadhara. Akiwa njiani kuelekea tarafa ya Mpimbwe ataona Mbuga
ya Wanyama ya Katavi ambapo ataweka jiwe la msingi katika Ghala la Stakabadhi
Mazao na kukabidhi hati za kimila za umiliki wa ardhi 300 katika kijiji cha
Mwamapuli.
Akiwa wilayani Nkasi kuanzia
tarehe 20 Februari 2012 Makamu wa Rais atapokea taarifa ya ujenzi wa barabara za
Mkoa wa Rukwa na taarifa ya Wilaya ya Nkasi. Atafungua miradi ya maendeleo
ikiwepo nyumba ya watumishi wa Halmashauri, Jengo la Utawala Shule ya Sekondari
Nkomolo, na Daharia Shule ya Sekondari Korongwe. Atafanya pia Mkutano wa hadhara
katika kiwanja cha shule ya Sekondari Korongwe.
Akimaliza ufunguzi wa miradi
hiyo, ziara yake itahamia katika Wilaya ya Sumbawanga ambapo atamalizia ziara
yake na kuelekea Mbeya kwa ajili kuendelea na zoezi kama hilo ambalo
linategemewa kufanyika katika nchi nzima.
Mhe. Makamu wa Rais atawasili
Sumbawanga tarehe 22 Februari 2012 akitokea Nkasi ambapo atapokelewa na viongozi
wa Chama na Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya. Baada ya kupokelewa atapewa
taarifa fupi ya Chama na Serikali.
Awapo Sumbawanga atapata fursa
ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo ataweka jiwe la Msingi Jengo
la ofisi ya Mkaguzi Mkazi Mkoa wa Rukwa na Jengo la benki ya CRDB.
Atazindua Maghala ya kuhifadhi bidhaa bandarini yaliyopo Kasanga, Soko Jipya la
Samaki Kasanga, na kampeni ya usafi katika Mji wa Sumbawanga “SUMBAWANGA NG’ARA”
kwa kugawa vitendea kazi vya usafi.
Atapata pia fursa ya
kusalimiana na wananchi katika maeneo yote ya miradi atakayotembelea ambapo
atatembelea pia ngome ya “FORT BISMARK” iliyopo Kasanga na Kiwanda cha nyama cha
SAAFI kinachomilikiwa na Mbunge Msataafu na mjasiriamali Ndugu Chrissant
Mzindakaya.
Makamu wa Rais pia atafanya
Mikutano wa hadhara katika viwanja vya Rukwa High School na Uwanja wa Mpira wa
Laela. Atazungumza na wazee maarufu wa Wilaya ya Sumbawanga katika uwanja wa
Ikulu Ndogo ya Sumbawanga.
Mhe. Makamu
wa Rais atakamilisha ziara yake tarehe 24/02/2012 na kuondoka Sumbawanga
kuelekea Mkoa jirani wa Mbeya ambapo atakuwa na ratiba ya ziara ya kikazi Mkoani
humo.
KUTOKA RUVUMA LEO: MAKAMU WA RAIS ATOA TAMKO KUHUSU MRADI WA URANIUM - NAMTUMBO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amewahakikishia wakazi wa mkoani Ruvuma na Tanzania kuwa
mradi wa mgodi tarajali wa Urani wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma utatekelezwa
kwani una umuhimu kwa taifa.
Amesema hayo wakati akiongea
na wafanyakazi wa mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Mantra Tanzania kuwa
serikali inafuatilia kwa makini kuona madini haya muhimu ya nalifaidisha
Taifa
Aliongeza kuwa anao uhakika
kuwa taratibu zote za hifadhi ya mazingira na usalama wa maisha ya wakazi wan
aozunguka eneo hilo umetiliwa mkazo nwa Kampuni kwa kushirikiana na taasisi ya
nishati ya atomiki Tanzania
.Aidha kwa upande wake
Mkurugenzi wa Mantra Tanzania Asa Mwaipopo ameiomba serikali kuharakisha
taratibu za kisheria ili mgfodi uweze kuanza hapo mwaka ujao kwa ujenzi na
ifikiapo 2014 uzalishaji uanze ili ajira zipatazo 1600 wakati wa ujenzi wa mgodi
na zingine 400 wakati wa uzalishaji ziweze kupatikana kwa watanzania na kusaidia
kukuza uchumi.
No comments:
Post a Comment