Tuesday, April 30, 2013

MOURINHO AFA KIUME SANTIAGO BERNABEU APIGA 2-0 LAKINI HAZITOSHI KUMSONGESHA FAINALI!!

Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Daah! Ali manusura vijana wa Mourinho waione Wembley mwaka huu baada ya kuwafunga nyuki wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani, Borrusia Dortmund mabao 2-0 usiku huu katika dimba la Santiago Bernabeu

Matokeo hayo yameitupa nje Real Madrid kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza nchini ujerumani ambapo Mourinho alipiga kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 4-1 na baada ya kushinda leo kwa mabo mawili Madrid wanatoka kwa wastani wa mabao 4-3.
Mchezo wa leo ulikuwa mgumu sana kwa Mourinho kwani walilazimika kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa 0-0 na kipindi cha pili kilipoanza bado mambo yalikuwa magumu mpaka dakika ya 83 ambapo waliandika bao la kwanza kupitia kwa Mfaransa Karim Benzema akipokea pasi nzuri kutoka kwa Mjerumani Mesut Ozil.
Na katika dakika ya 88 beki machachari Sergio Ramos alimalizia pasi maridhawa ya Karim Benzema na kuzamisha gozi kambani, lakini matokeo hayo hayajafua dafu kufuatia kipigo cha 4-1 ugenini. 

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo Real Madrid walicheza vizuri zaidi ya wapinzani wao lakini walishindwa kupangua ngome imara ya Kocha Flopp aliyetamba toka awali kuwa hawataweza kuwafunga, lakini kipindi cha pili waliachia na kufungwa, kama Madrid wangekuwa makini wangewatoa leo baada ya kupoteza nafasi muhimu.
Ozil hatasaulika kwa mashabiki wa soka wa Real Madrid baada ya kupoteza nafasi muhimu za kufunga mabao ambayo yangewapeleka dimba la taifa la Wembley nchini Uingereza kucheza mchezo wa fainali.

Waswahili wana msemo wao usemao “Mwenzako akinyolewa zako tia maji”, Madrid safari yao imekwisha leo usiku huku wakiathiriwa na matokeo ya mchezo wa kwanza, watani zao wa jadi, FC Barcelona nao kesho wanapambana na Wekundu wa kusini mwa Ujerumani FC Bayern Munich katika dimba la Camp Nou huku Barca wakiwa na kumbukumbu ya kutandikwa mabao 4-0  Allianz Arena.

Je yatawafika ya Madrid leo ama watafunga mabao 5-0 ili wafuzu fainali na hatimaye kukutana na Dortmund ambao wameshakata tiketi leo usiku.
Delicately poised: Robert Lewandowski attempts to play the ball with the back of his foot 
Muuaji Robert Lewandowski akijaribu kupiga mpira kwa utalaamu mkubwa
Is it on? Sergio Ramos makes it 2-0 and gives Madrid hope  
Sergio Ramos akishangilia bao lake la pili lililowapa Madrid Matumaini makubwa
VIKOSI VYA TIMU ZOTE
Real Madrid: Diego Lopez, Essien, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain.
Subs: Casillas, Pepe, Khedira, Kaka, Benzema, Albiol, Morata.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Bender, Blaszczykowski, Gotze, Reus, Lewandowski.

Subs: Langerak, Kehl, Leitner, Sahin, Grosskreutz, Schieber, Felipe Santana.
Mwamuzi: Howard Webb
Smashing it home: Ramos sets up a grand stand finish with a late strike  
Ramos akitandika mkwaju mkali kwa guu la dhahabu kwa wanasoka, guu la kushoto 
In with a shout: Benzema gets Madrid's first
Benzema akiandika bao la kwanza
Wrestle for the ball: Real Madrid players fight with Dortmund's goalkeeper Roman Weidenfeller after the first goal 
Wachezaji wa Real Madrid wakimtaka kipa wa Dortmund Roman Weidenfeller asimame baada ya kufunga bao la kwanza kwani alionekana kutka kupoteza wakati
Not enough: Cristiano Ronaldo was unable to help Madrid make the Champions League final  
Haikutosha: Cristiano Ronaldo hajaweza kuisadia Madrid kufika fainali ya UEFA mwaka huu
Going close againL Dortmund's danger man Robert Lewandowski sees his effort go wide  
Robert Lewandowski akichungulia moja ya mashuti yake kama unaingia kimiani ama la
No way though: Real Madrid's Gonzalo Higuain vies for the ball with Mats Hummels  
Hakuna Ujanja: Nyota wa Real Madrids Gonzalo Higuain  akijaribu kumpokonya kipa Mats Hummels
High jump: Lewandowski fights for the ball with Raphael Varane  
Wakiruka juu zaidi: Lewandowski akipigania mpira na beki wa Madrid Raphael Varane
Down and out: Ronaldo gestures after being knocked to the floor 
Ronaldo akionekana akilalamika baada ya kuungashwa
No way Jose: Mourinho shows his frustration on the sidelines 
Hana jinsi: Mourinho akionekana amepaniki sana
End of the road: Ronaldo walks on the pitch looking dejected 
Mwisho wa safari: Ronaldo akitembea uwanjani akionekana amechanganyikiwa na mwenye mawazo baada ya filimbi ya mwisho

No comments:

Post a Comment