Dar es Salaam. Wamiliki wa
Vyombo vya Habari nchini wametakiwa kutoa mafunzo ya kujihami na maadui
kwa waandishi wa habari pamoja na mafunzo ya kuwajengea misingi na
maadili ya uandishi bora wa kazi zao.
Hatua hiyo inatokana na mfululizo wa matukio ya kutekwa, kuteswa na vitisho dhidi ya baadhi ya waandishi wa habara hapa nchini.
Akizungumza kwenye mkutano wa Wadau wa Habari,
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi Habari Wanawake Tanzania
(Tamwa), Valerie Msoka alisema, ipo haja sasa kwa wamiliki wa vyombo vya
habari kutoa mafunzo kwa waandishi ili wawe na uwezo wa kujihami kwa
hali ilivyo sasa.
Msoka alisema kwa jinsi hali ilivyo sasa ni vyema
pia waandishi wakapewa mafunzo ambayo yanawapa mbinu jinsi gani wanaweza
kupambana na misukosuko wakati wanapokuwa ndani na nje ya mahali pa
kazi.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, mbali na mafunzo
hayo hali ya usalama pia kwa waandishi bado ni kitendawili hapa nchini,
hivyo wamiliki wanatakiwa kuwahakikishia usalama wao kikazi na
kimahitaji.
Kwa upande wake, Profesa Nicholls Boas kutoka Chuo
Kikuu cha Maryland Marekani, aligusia suala la mfumo wa vyama vingi
kuwa ni changamoto kwa vyombo vya habari kutokana na kuweka mambo
yaliyojificha wazi.
No comments:
Post a Comment