Thursday, July 5, 2012

Waziri Mkuu Kuanza Ziara Ya Mkoa Wa Ruvuma Kesho


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Thabit Mwambungu akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kuanza kwa ziara ya Waziri Mkuu katika mkoa wa Ruvuma hapo kesho.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu anawatangazia wananchi wa mkoani Ruvuma kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda (Mb) atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Ruvuma kuanzia kesho tarehe 06 Julai 2012 hadi tarehe 07 Julai 2012.

Akiwa mkoani Ruvuma Mheshimiwa Waziri Mkuu atafanya kazi ya kuzindua kampeni ya Kimkoa ya matumizi ya matrekta makubwa katika kilimo ili kuhamasisha Jamii kutumia zana bora za kuongeza uzashalishaji wa mazao na hatimaye kuinua uchumi wa wananchi.

Aidha katika ratiba ya ziara hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu atapokea taarifa ya mkoa ya shughuli za maendeleo , taarifa ya maendeleo ya Chama Tawala CCM ,atapokea taarifa ya shamba na kukagua maandalizi ya kilimo cha kahawa katika kijiji cha Lipokera na hatimaye atapata fursa ya kuongea na wananchi wa mkoa wa Ruvuma kupitia wananchi wa Manispaa ya Songea katika viwanja vya Zimanimoto.


Wito unatolewa kwa wananchi wa Manispaa wa Ruvuma na vitongoji vya jirani kujitokeza kwa wingi katika kumlaki na kumsikiliza Waziri Mkuu atakapowasili na akapokuwa katika maeneo ya kazi kama ratiba yake inayoonyesha.

Imetolewa naRevocatus A.KassimbaAfisa HabariOfisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma: 05 Julai 2012.

No comments:

Post a Comment