Wednesday, July 25, 2012

Tanzania Yashiriki Mkutano Wa Kimataifa Juu Ya Afya Ya Damu - Paris Ufaransa



Na: Richard Minja kutoka Paris Ufaransa

Mkutano wa shirikisho la WFH umefanyika Paris Ufaransa ambapo umehudhiriwa na nchi takribani 86 kati ya 120 zinazounda shirikisho hilo. Tanzania imewakilishwa na Mr. Richard Minja wa Chama cha watu wenye Hemophilia.
Hemofilia ni ugonjwa unaopata mzaliwa 1 kati ya 1,000 wanaume na wanawake ambapo damu yao hukosa uwezo wa kuganda pale mshipa unapochanika. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kujaza pengo kati ya wapatao na wasiopata matibabu na huduma bora duniani. Ugonjwa huu una hatari ya kusababisha vifo, ulemavu na maumivu makali.

No comments:

Post a Comment