Brass Band ya JWTZ ikijiandaa tayari kwa Gwaride la Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye Viwanja vya Garden mjini Iringa.
Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Iringa, Afande Shayo, akitoa maelekezo kabla ya tukio la kuwakumbuka mashujaa kuanza.
Usishangae kukuta maganda ya risasi pale Garden, ndizo heshima hizo zinatolewa. Paaaa! Unaweza kukimbia.
Mnara wenye orodha ya majina 56 ya mashujaa waliopoteza wa Wilaya ya Iringa maisha wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kati ya mwaka 1939 hadi 1945.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akiweka Ngao kwenye Mnara wa Kumbukumbu.
Chifu Abdul Adam Ssapi Mkwawa akiweka Upendi na Mishale.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi, akiweka shada la maua.
Ngojeni nikanywe maji jamani, nimesimama kwa saa tatu hivi nikisubiri sherehe kuanza, si mnajua ratiba zetu zilivyo? Ukisikia inaanza saa mbili, basi ujue ni saa sita!
DM
No comments:
Post a Comment