Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbalimbali vya Habari Nchini kuhusiana na Vurugu Zilizotokezea Zanzibar,hapo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Ukiwa ni Utaratibu wake wa kuzungumza na Vyombo vya Habari kila ifikapo mwisho wa Mwezi.
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya vurugu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar jana,Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote,atakayethubutu kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”
Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji wa stamp ya uvumilivu wa kidini.
“Kwa masikitiko makubwa nataka kusema kuwa vitendo vilivyotokea vya kuvunja amani ni vya aibu, vimetusononesha sana na haya wananchi lazima wajue kuwa amani yetu ni muhimu kuliko jambo lolote lile” Alisema Rais Dk. Shein.
No comments:
Post a Comment