Sunday, April 1, 2012

Mapokezi makubwa yakumkaribisha Mkuu Mpya wa Mkoa wa Katavi

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh: Joyce Mgana akiwapokea wakuu wa mikoa ya Katavi na Rukwa katika eneo la Kizi lililopo katikati ya Mkoa wa Rukwa na Katavi

Mtu maarufu katika kabila la wasukuma ajulikanaye kwa jina la "Mchoma Simba" ambaye huveshwa mavazi hayo baada ya kuua Simba kama ishara ya ushujaa akicheza ngoma mbele ya uongozi wa Mikoa ya Rukwa na Mkoa Mpya wa Katavi kwenye makabidhiano ya Mkoa huo jana. Mkoa wa Rukwa umegawanywa na kuundwa Mkoa Mpya wa Katavi ikiwa ni jitahada za Serikali katika kusogeza huduma kwa wananchi wake. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana.
Mburudishaji huyo wa Kisukuma akiendelea kufanya vitu vyake
Baadhi ya watumishi kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa ikongozwa na Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Utawala na Rasilimali Watu Samson Mashalla, Afisa Tawala Festo Chonya na Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa Rukwa Frank Mateni wakiangalia burudani ya Mchezaji huyo wa Kisukuma.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akiwatambulisha baadhi ya viongozi waliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa Wananchi wa Wilaya ya Nkasi katika Kijiji cha Kizi waliokusanyika kumuaga Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe jana.
Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa ikiwa imejipanga tayari kushuhudia Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe (hayupi pichani) kwa baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa Mpya wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akisalimiana na Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa Mpya wa Katavi waliojitokeza kumpokea baada ya kukabidhiwa kwao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, kwa pamoja waliongozana kuelekea Katavi kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya Mkoa huo Mpya wa Katavi.
Hapa ni Mpakani mwa Mikoa ya Rukwa na Katavi kwenye Mlima maarufu wa Lyamba Lyamfipa. Utawala wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya unaishia hapa, anashusha kibendera kuruhusu Utawala Mpaya wa Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe kupandisha bendera yake tayari kuipepeza kwenye Milima na Mabonde ya Utawala wake Mpya wa Mkoa Mpya wa Katavi. 
Bendera ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya imeshashushwa.
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akiwa tayari kupepeza bendera yake kwa mara ya kwanza katika Mkoa wake mpya wa Katavi baada ya kukabidhiwa Mkoa huo jana. 

Picha ya pamoja ya viongozi wa mikoa ya Rukwa na Katavi kutoka kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh:Joyce Mgana, wa pili toka kushoto ni Mh: Inginia Stella Manyanya Mkuu wa mkoa wa Rukwa, watatu kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh: Dkt Rajabu Rutengwe na wa mwisho kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bw Alhaj Salum Mohammed Chima
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akimtambulisha kwa mara kwanza mkuu mpya wa mkoa wa katavi kwa wananchi wa kijiji cha kizi


Kutoka Kulia ni Mkuu  Mpya wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe, Anayefuata katikati ni  Injinia Emmanuel Kalobelo Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi na  wa mwisho kutoka kulia ni Alhaj Salum Mohammed Chima Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa wakifuatilia moja ya matukio katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Mkoa Mpya wa Katavi


Inginia Emmanuel Kalobelo akimshukuru mwenyezi mungu wa kuteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Mpya wa Katavi na akijitambulisha kwa wananchi wa kijiji cha Kizi na kupiga hodi katika Mkoa mpya wa Katavi 

Baadhi ya Viongozi wa vyama na Serikali wakishuhudia nao makabidhiano katika ya mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Katavi  katika kijiji cha Kizi Mpakani mwa Mikoa hiyo

Bw. Betuely Ruhega ambaye ni Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi akishuhudia makabidhiano katia ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa na Katavi katika kijiji cha Kizi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh Injinia Stella Manyanya akiongoza Ibada katika Kijiji cha kizi

Viongozi wa Mkoa Mpya wa Katavi injinia Emmanuel Kalobelo kutoka kushoto ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi na anayefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh Dkt Rajabu Rutengwe wakimshukuru Mwenyezi Mungu katika Ibada fupi iliyoongozwa na Mh Injinia Stella Manyanya 


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Inginia Stella Manyanya akishusha Bendera yake ya Mkoa wa Rukwa na Kuruhusu kupandisha Bendera ya Mkuu wa Mkoa Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh: Inginia Stella Manyanya akimuonyesha mpaka wa Katavi na Rukwa Mh: Dkt Rajabu Rutengwe
Mh Injinia Stella Manyanya akiwashukuru wananchi wa kata ya Sitalike kwa Mapokezi yao mazuri ya kumpokea Mkuu wa Mkoa wa Katavi


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh: Inginia Stella Manyanya akiwatambulisha viongozi wa Mkoa mpya wa Katavi Mh Dkt Rajabu Rutengwe ambaye ndiye Mkuu wa mkoa wa Katavi na Injinia Emmanuel Kalobelo ambaye naye ndiye Katika Tawala wa Mkoa wa Katavi


Viongozi wa Mkoa Mpya wa Katavi Injinia Emmanuel Kalobelo ambaye hajavaa miwani ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi na anayefuata ni Mh Dkt Rajabu Rutengwe ambaye ndiye Mkuu Mpya wa Katavi


Mh Dkt Rajabu Rutengwe ambaye ndiye Mkuu Mpya wa Katavi akiwasalimu wananchi wa Kata ya Sitalike alipopokelewa na wananchi hao jana


Mh Dkt Rajabu Rutengwe ni Mkuu Mpya wa Mkoa wa  Katavi akimtambulisha kwa wananchi Injinia Emmanuel Kalobelo katika Kata ya Sitalike walipopokelewa na wananchi hao jana


Mh Dkt Rajabu Rutengwe ambaye ni  Mkuu wa Mkoa wa Katavi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Sitalike huku akiwambia kuwa wanamwaka mmjoa na miezi kumi na tisa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 huku akiwataka ushirikiano wao ili kuweza kuujenga Mkoa huu Mpya wa Katavi jana


Baadhi ya Viongozi wa Serikali na vyama mbalimbali wakisikiliza hutuba iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika kata ya Sitalike


Mh Injinia Stella Manyanya akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Kashaulili ambapo ndipo palipofanyika mkutano pamoja na kuwatambulisha viongozi wa Mkoa Mpya wa Katavi


Mh Dkt Rajabu Rutengwe ambaye ndiye Mkuu Mpya wa Mkoa wa Katavi akiwapungia wananchi wa Mpanda Mjini alipowasili katika uwanja wa Kashaulili alipokuwa anaenda kuwahutubia wananchi kabla ya kushuka kwenye gari lake 


Katibu Tawala wa Mkoa Mpya wa Katavi Injinia Emmanuel Kalobelo akiwasili katika uwanja wa Kashaulili


Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh Dkt Rajabu Rutengwe akishuka kwenye gari lake mara baada ya kuwasili katika uwanja wa kashaulili huku akielekea kwenda kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma toka mjini hapa Mpanda


Mh Dkt Rajabu Rutengwe ambaye ndiye Mkuu Mpya wa Mkoa wa Katavi akikagua kwaya ambayo ilikuwa ikitumbuiza uwanjani hapo


Mh Dkt Rajabu Rutengwe ambaye ndiye Mkuu Mpya wa Mkoa wa Katavi akikagua kikundi cha ngoma
za asili kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo
Mh Dkt Rajabu Rutengwe Mkuu wa mkoa wa Katavi akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali kuelekea jukwaa kuu


Mh Dkt Rajabu Rutengwe Mkuu wa mkoa wa Katavi na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh Injinia Stella Manyanya wakisaini vitabu vya wageni uwanjani hapo  


Viongozi wa Madhehebu mbalimbali wakiomba dua la kumuombea  mkuu wa mkoa wa Katavi na kumuombea afya njema na aendelee kutenda kazi ya kumpendeza mwenyezi mungu sikun zote.


Kwa ya Vijana Moraviani wakituimba katika uwanja wa Kashaulili kuombea amani Tanzaniaa na katika Mkoa Mpya wa katavi


Injinia Emmanuel Kalobelo ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi akisaini Vitabu vya wageni  katika Uwanja wa Kashaulili.


Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akikabidhiwa uchifu wa kabila la wabende na Chifu wa Kabila hilo Victor Mfinula katika uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda jana. Kushoto anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

Mkuu wa mkoa wa Katavi  Dkt Rajabu Rutengwe  akiwa anakabidhiwa zana za jadi na chifu wa kabila la wabende katika uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe  akiwa amekabidhiwa zana za jadi na chifu wa kabila la wabende akimpatia maelekezo jinsi ya kutumia za hizo za jadi katika uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe  akiwa anakisomewa risala na moja wa chifu wa kabila la wabende katika uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda
Mwenyekiti wa Chama Wilaya Bw: Sebastiani Kapufi akisoma maelezo yaliyopo kwenye cheti walichomzawadia Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika uwanja wa kashaulili Mjini Mpanda


Mkuu wa Mkoa wa Katavi akipokea Cheti cha Heshima alichozawadiwa na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mpanda na kukionyesha mbele ya wananchi waliofika katika uwanja huo wa kashaulili Mjini Mpanda


Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw. Kanoni akiwasilimia wananchi katika uwanja wa Kashaulili na Kuwakaribisha viongozi wa Mkoa pamoja na wale wa vyama na Serikali katika uwanja wa kashaulili Mjini Mpanda
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh Joyce Mgana akiwasalimia wananchi wa Mkoa Mpya wa Katavi katika uwanja wa kashaulili mjini Mpanda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mjini


Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Akiwasalimia wananchi wa mjini Mpanda katika Mkoa Mpya wa Katavi na kuwashukuru kwa kuweza kufika uwaanjani hapo kuwalaki viongozi wao wa Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwatambulisha viongozi wa Mkoa wa Katavi  mbele ya wananchi waliofika uwanjani hapo katika uwanja wa kashaulili mjini Mpanda 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabizi diare (notebook) Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe katika uwanja wa kashaulili mjini Mpanda


Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Injinia Emmanuel Kalobelo akiwasilimia wananchi wa Mkoa Mpya wa Katavi baada ya utambulishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika uwanja wa Kashaulili


Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akihutubia wananchi wake wa Mkoa Mpya wa Katavi mara baada ya kutambulishwa kwao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Aliwaahidi ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha Katavi inasonga mbele.


Dkt Rajabu Rutengwe Mkuu wa mkoa wa Katavi akimtambulisha Katibu wake wa Mkoa Bw. Betuely Ruhega katika Uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda 


Viongozi mbalimbali wakishuhudia makabidhiano hayo katika ikulu ndogo Mjini Mpanda Mkoani Katavi


Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bw. Chima akisaini na kumkabidhi Taarifa za Mkoa wa Katavi Injinia Emmanuel Kalobelo katika Ikuli Ndogo Mjini Mpanda Mkoani Katavi


 Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bw. Chima akimkabidhi Taarifa za Mkoa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Injinia Emmanuel Kalobelo katika Ikuli Ndogo Mjini Mpanda Mkoani Katavi


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe wakisaini makabrasha ya makabidhino ya Mkoa Mpya wa Katavi jana usiku katika Ikulu ndogo ya Katavi mara baada ya Mkoa wa Rukwa kugawanywa na kuundwa Mkoa Mpya wa Katavi ikiwa ni jitihada za Serikali kusogeza huduma kwa Wananchi wake. Hapo awali kabla ya kuteuliwa Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Taarifa za Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe  katika Ikuli Ndogo Mjini Mpanda Mkoani Katavi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Injinia Emmanuel Kalobelo akiwashukuru wananchi waliohudhuria tafrija fupi iliyoandaliwa katika Ikuli Ndogo Mjini Mpanda amakoani Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa taarifa za Mkoa wa Katavi na Rukwa katika Ikulu ndogo iliyopo Mkoani Katavi

 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe akiwashukuru wananchi waliohudhuria tafrija fupi iliyoandaliwa katika Ikuli Ndogo Mjini Mpanda amakoani Katavi
Wazee wa Mkoa wa katavi wakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali katika Ikulu ndogo ya Mkoa mpya wa Katavi

No comments:

Post a Comment