WAZIRI
MKUU WA TANZANIA MIZENGO PINDA
RAIS WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO
KAMANDA
WA POLISI WA MKOA WA MBEYA ADVOCATE NYOMBI
JESHI la polisi mkoani Mbeya
limeendelea kujisiriba matope kwa kuendesha mauaji ya kiholela kwa raia ambapo
jana askari wa jeshi hilo wamemuua mwanafunzi Said Msabaha wa shule ya Sekondari
Lupa iliyopo wilayani Chunya mkoani hapa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lupa
wilayani humo William Patrick Mbawala, ameuambia mtandao huu wa kijamii kuwa mwanafunzi huyo kabla ya kifo chake alikamatwa na
askari hao akiwa na wenzake watatu kwa tuhuma za wizi wa simu Februari 29, mwaka
huu na baadaye waliachiwa kwa dhamana.
Amesema baada ya kutolewa katika
kituo kidogo cha Lupa, Marehemu alionekana kuwa hali yake imedhoofika na
alipoulizwa alieleza kuwa alipokuwa kituoni hapo alipigwa na askari polisi jambo
ambalo liliwalazimu kumpeleka katika zahanati ya kijiji hicho chini ya Mganga
aliyemtaja kwa jina la Dr. Solomon.
Amesema Baada ya kuona hali yake
inaendelea kuwa mbaya ndipo lilipochukuliwa jukumu la kumpeleka Hospitali ya
wilaya na bahati mbaya akafia njiani hata kabla ya kumfikisha katika Hospitali
hiyo.
Naye Baba mzazi wa marehemu,
Msabaha Hussein, amesema kuwa baada ya kufariki mtoto wake akachukua jukumu la
kupeleka maiti kituo cha polisi ili wahusike katika kuuzika mwili wa marehemu
kwa kile aichodai kuwa kifo cha mwanae ni matokeo ya kipigo walichokitoa
alipokuwa mikononi mwao.
Nao baadhi ya wananchi
waliohojiwa kwa masharti ya kuhifadhi majina yao wamesema kuwa baada ya kuona
hali hiyo na kwasababu askari wanaodaiwa kuhusika wanawafahamu ndipo
walipochukua jukumu la kuwatafuta askari hao ambao tayari walikuwa wametokomea
kusikojulikana.
Wamesema kuwa baada ya kuwakosa
katika makazi yao, waliamua kuzichoma moto nyumba za askari hao ambao ni Copl.
Maxmillian, PC Mjuni na PC Hery ambapo hawakuishia hapo walimtafuta PC Fadhil
bila mafanikio na kuharibu samani zake za ndani huku wakishinikiza Jeshi la
polisi kuuzika mwili wa marehemu huyo.
Afisa upepelezi wa Jeshi hilo
mkoani Mbeya (RCO) Elias Mwita alipotakiwa kuzungumzia sakata hilo alisema kuwa
ni mapema mno.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wilayani Chunya Deodatus Kinawiro ambaye ni Mkuu wa wilaya hiyo
alipotafutwa ili aweze kuzungumzia tukio hilo hajaweza kupatikana kupitia simu
yake ya kiganjani.
Awali askari hao walidaiwa
kutorokea Jijini Mbeya lakini taarifa kutoka ndani ya vyanzo vya kikosi kazi cha
blogu hii ya kalulunga.blogspot.com jeshi la Polisi mkoani Mbeya vimesema kuwa
askari hao walikuwa bado hawajakamatwa wala kuonekana katika viunga vya Jiji la
Mbeya.
Tukio hilo la kinyama limetokea
siku chache baada ya askari wa jeshi hilo PC Maduhu kuhusika kumuua aliyekuwa
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya Daniel Godluck Mwakyusa
(31) February 14, mwaka huu
No comments:
Post a Comment