Monday, March 5, 2012

Msimamo Wa Madaktari Leo


05/03/2012
KAMA TULIVYOTOA TAARIFA KWENYE KIKAO CHA MADAKTARI CHA MARCH
3, NI KWAMBA

MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA NA HATIMAYE KUTIWA SAINI KATI YA
SERIKALI NA
MADAKTARI TAREHE 2/3/2012 NI KUWA, ILI MEZA YA MAZUNGUMZO YA KUJADILI
MADAI
YA MADAKTARI IWEZE KUENDELEA NA HATUA YA PILI NI LAZIMA WAZIRI WA AFYA
(DR MPONDA) NA NAIBU WAKE (DR LUCY NKYA) AMA WAJIUZULU AU WAWAJIBISHWE
KAMA

ILIVYOKUWA IMEAHIDIWA NA MH. WAZIRI MKUU FEBRUARY 9 ALIPOFANYA KIKAO
NA WATUMISHI WA AFYA PALE HOSPITALI YA MUHIMBILI.

AIDHA, KULINGANA NA MAKUBALIANO HAYA KIKWAZO KIKUBWA CHA
KUTOKUENDELEA KWA MAJADILIANO YA MADAI YA MADAKTARI (UBORESHAJI
WA HUDUMA WAPATAZO WAGONJWA,

MAZINGIRA MAZURI YA KUFANYIA KAZI NA MASLAHI KWA UJUMLA WAKE) NI
KUENDELEA KUWEPO KWA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA KWENYE NAFASI ZAO ZA
KIUONGOZI.

HIVYO BASI, KWENYE HUO MKUTANO WA MARCH 3, BAADA YA MAJADILIANO NA
TAFAKARI ZA KINA, ILIKUBALIWA KWA PAMOJA KUWA WATU HAWA WAWILI
WANATAKIWA KUACHIA NGAZI MARA MOJA ILI HAKI ZA WAGONJWA
NA MADAI YA MADAKTARI YAWEZE KUJADILIWA NA KUTEKELEZWA.

HIVYO BASI, ILIAMULIWA KUWA KAMA MPAKA SIKU YA JUMATANO
(MARCH 7) BADO AKINA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA WATAKUWA BADO WAPO
MADARAKANI WATAANZA MGOMO RASMI KUSHINIKIZA AMA WAJIUZULU AU
WAWAJIBISHWE ILI TARATIBU ZINGINE ZIWEZE KUANZA.

KAMA ILIVYO TARATIBU YA CHAMA KUTOA TAARIFA KWA WANACHAMA KOTE NCHINI,
IFAHAMIKE KWAMBA MKUTANO ULIAMUA KUWA MADAKTARI WOTE KUWA KUANZIA
JUMATANO (MARCH 7) WATASITISHA KUTOA HUDUMA ZOTE ZA AFYA KATIKA
HOSPITALI ZOTE NCHINI MPAKA HAPO SERIKALI ITAKAPOONESHA UTAYARI KWA
KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUWAWAJIBISHA WATAJWA HAPO JUU ILI HATUA
ZINGINE ZA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI KWA MANUFAA YA TAIFA
YAWEZE KUANZA KUSHUGHULIKIWA.

IFAHAMIKE KWAMBA CHAMA KINASIKITISHWA SANA NA KITENDO
CHA VIONGOZI WAANDAMIZI WA WIZARA YA AFYA AMBAO WANAJUA
UMUHIMU WA KUWAJIBIKA. KWA MARA NYINGINE TENA WANAWAFANYA
MADAKTARI WAENDELEE KUTETEA HAKI ZA WATANZANIA

KATIKA NJIA NGUMU NA KWA NIA YA KUFANIKISHA MALENGO HAYA KWA FAIDA YA
WATANZANIA WOTE.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAT MAKAO MAKUU.


DR. NAMALA MKOPI RAIS WA MAT

No comments:

Post a Comment