Tuesday, March 6, 2012

MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengweakifanya ziara yake ya siku tatu kutembelea kata zote zilizopo Halmashauri ya Mji Mpanda akiwa na Mwenyekiyi wa Halmashauri hiyo Mh: Enock Gwambasa akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa Halmashauri hiyo na wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo ya Mji
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mpanda Mh: Enock Gwambasa akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu Halmashauri yake ya Mji na wanavyojiandaa kuupokea mkoa mpya wa Katavi.

Afisa mapato wa wilaya ya Mpanda Bw. Sitta akitoa taarifa juu ya ukusanyaji mapato katika halmashauri na kutoa elimu juu ya umiliki wa vyombo vya moto na namna ya kujiunga na kumiliki tini kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili Mji na Wilaya

Bw. Ladislaus Bamanyisa akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya na kujitamblisha kwa wananchi kuwa yeye ni Afisa meneja wa nyumba Mkoa wa Katavi na Rukwa kata ya Ilembo namna ya ujenzi bora wa nyumba za kuishi 

Afisa mipango miji wa Halmashauri ya mji Mpanda Bw Kaswa akijibu maswali kwa ufasaha juu ya swala zima la ardhi kwa wafugaji na kuwaelekeza namna ofisi yao ya ardhi ilivyo jipanga  katika swala zima la mipango miji

Bi Merry Afisa Mtendaji wa kata ya Ilembo akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya kuhusiana na kata yake hiyo  juu ya uendeshaji wa kata hiyo na kutoa taariufa juu ya wanafunzi waliofauli kujiunga na kitato cha kwanza mwaka huu na waliofeli katika kata yake. 

Mzee wa kata ya Ilembo ambaye jina lake hatukuweza kulitambua mara moja akiuliza swali juu ya ardhi walio itoa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Ilembo na kudai malipo yao

Afisa mtendaji Bw Mashauri akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wananchi wa kata katika  mkutano wa mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Rajabu Rutengwe juu ya wafugaji na wakulima waliohamia katika kata hiyo na kueleza hatua zilizofikia katika kutatua tatizo hilo la wahamiaji

No comments:

Post a Comment