Mkurugenzi wa Utawala LAPF Taifa Bwana Singoda akifungua mafunzo.
Mafunzo hayo yaliyofanyika Mkoani Mbeya katika ukumbi wa Mbeya Paradise Inn yalishirikisha wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya.Idara zilizoshiriki katika mafunzo hayo ni Idara za Utumishi,Fedha,TSD,Vyama vya Wafanyakazi na Mashirika mbalimbali.Mfunzo hayo yaliongozwa na Mkurugenzi wa Utawala Bwana Sigonda kutoka makao makuu ya LAPF Dar es salaam.
Mada mbalimbali zilizo jadiliwa ni Historia ya mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania,Sheria ya Hifadhi ya jamii ya mwaka 2008 (The social security act, 2008), Uanzishwaji wa Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Sekta ya hifadhi ya jamii,Shughuli za uandikishaji wa wanachama na ukusanyaji wa michango na Maandalizi ya kustaafu.
Wadau mbalimbali kutoka mikoa iliyotajwa hapo juu baada ya kupata mafunzo hayo walihojiwa na mwadishi wako wamepokea vipi mafunzo hayo? Wengi waliusifu mfuko wa wa Hifadhi ya jamii LAPF kwa uamuzi waliofafanya maana wamefunguliwa vichwa vyao kwa kuwa mambo mbalimbali wamejifunza yanayofanywa na mfuko huo kwa kufuata miongozo iliyowekwa kisheria na nchi yetu.Pia moja ya pangezi nyingine ni ilitolewa kotokana na huduma inayotolewa kwa mwanachama wa kike atakayekuwa amejifungua kwa kumpa kiasi fulani cha fedha ambapo ili aweze kujikimu ikiwa katika mifuko mingine ya jamii huduma hii haipo.
Mwisho wadau walitoa maswali mbalimbali yaliyoweza kujibiwa na watendaji wa LAPF kikamilifu.Pia wadau waliweza kotoa ushauri kwa mfuko mambo mbalimbali ili waweze kuuboresha mfuko kwa ustawi wa wanachama wao na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment