Sunday, February 26, 2012

Tohara Bure Kwa Wanaume Wote Wilayani Mpanda Mkoani Katavi


Dr Abdallah akiwa na kijana mwenye umri wa miaka ishirini na nne (24)
 baada ya kumaliza kumfanyia Tohara
Huwezi amini! Nimetembelea Hospitali ya Wilaya Mpanda na kukutana na foleni kubwa ya vijana, watoto na akina mama walioleta watoto wao wa kiume kufuatia tangazo la Tohara kwa wanaume wote Wilayani hapa!. Jambo lililonishangaza ni kuona kuwa bado kuna vijana na watu wazima wengi sana walikuwa  hawajafanyiwa Tohara katika wakati huu ambao huwa tunafikiri kuwa kila mwanaume hasa aishie mjini ametahiliwa kumbe si kweli kwa mujibu wa Dr.Josia chaula  ambae ndie mratibu wa zoezi hili  la Tohara. Anasema zoezi hili ni la wiki moja ambalo lilianza tarehe 20/02/2012 na litamalizika Tarehe 04/03/2012.
 Limelenga kufanya Tohara kwa watoto kuanzia miaka kumi na kuendelea ili kuweza kupunguza ongezeko la maambukizo ya magonjwa ya zinaa. Nilipomuuliza ni kwanini kuanzia miaka kumi nasio chini ya hapo?
Alijibu kuwa wamelenga umri huo kwakua ni umri ambao unapelekea vijana wengi kuanza kubarehe na wengine tayari wamekuwa wamebalehe na wameanza kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi ili kupunguza kasi ya maambukizo.
Pia alitoa wito kwa vijana kuendelea kujitokeza ili waweze kupatiwa huduma hiyo bure mpaka tunatoka eneo la tukio la hospital hiyo tulikuwa bado hatupata idadi kamili ya vijana waliojitokeza. Aliahidi kutupatia takwimu hizo baada ya zoezi hili kukamilika.



No comments:

Post a Comment