Bw. Niconemus Waivyala Mwenyekiti wa chama cha walimu Wilaya ya Mpanda akiwa ofisi kwake akitoa taarifa kwa walimu wa wilaya hiyo kuhusiana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
Akiwa ofisi kwake Bw. Waivyala aliwaeleza waalimu kuwa tamko la baraza la Taifa la chama cha waalimu Tanzania lililoazimia mambo mbalimbali likiwemo hili la nyongeza ya Mishahara ya Walimu kwa mwaka ujao wa fedha kuanzia Julai, 2012 vyanzo vipya vya mishahara viwe kama ifuatavyo:-
- Mwalimu wa cheti (Daraja A ) aanze na mshahara si chini ya Tsh. 500,000/= sawa na ongezeko la asilimia 100
- Mwalimu wa Stashahada aanze na mshahara si chini ya Tsh. 750,000/= sawa na ongezeko la asilimia 100
- Mwalimu mwenye shahada aanze na mshahara si chini ya Tsh. 938,000/= sawa na ongezeko la asilimia 100
Baraza laTaifa limeagiza kuwa majadiliano kuhusu nyongeza hii ya mshahara ianze mara moja na yawe yamekamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi 2012 ili Serikali iingize makubaliano hayo kwenye bajeti yake ya Mwaka 2012 wa fedha
No comments:
Post a Comment