Bunge la Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa siku
moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya
Madola kanda ya Afrika (CPA Africa). Mkutano huo utakaofanyika Mjini Arusha,
kesho tarehe 24 Februari, 2012, ambapo kamati hiyo ya CPA Africa, inakutana
nchini kujadili maswala mbalimbali ya chama hicho kwa kanda ya Afrika. Bunge la
Tanzania ndio makao makuu ya chama hicho kwa kanda ya Afrika
Kamati hiyo itahudhuriwa na wajumbe wa kamati tendaji
ambao ni:
Mhe. Rose Mukantabana (Mb) Rais wa Chama hicho kwa
kanda ya Afrika na pia ambaye ni Spika wa Bunge la Rwanda
Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) Mwenyekiti wa kamati ya
Utendaji wa Chama hicho ambaye pia ni Spika wa Bunge la Afrika
Kusini
Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) Makamu wa Rais wa CPA Afrika
na pia ndiye Spika wa Jimbo la Gauteng, nchini Afrika Kusini
Mhe. Request Mutanga (Mb) Muweka Hazina wa CPA Afrika,
na Mbunge kutoka Bunge Zambia
Mhe. Job Ndugai (Mb) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania,
ambaye pia ndiye mwenyeji wa kamati hiyo hapa nchini,
Na Dr. Thomas Kashililah, Katibu wa Kanda wa chama
hicho ambae pia ni katibu wa Bunge la Tanzania
Tanzania imekuwa makao makuu ya Kanda ya CPA Afrika
tangu mwaka 2004, ambapo shughuli zote za chama hicho huratibiwa na sekretariat
ya CPA ambayo ipo nchini Tanzania.
Imetolewa na Ofisi ya Bunge
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa
Kimataifa
24, Februari, 2012
DAR ES SALAAM
Dk. Shein Awapongeza Halaiki
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akipeana mikono na kuwapongeza Walimu
wa Mchezo wa Halaiki ambao walifanikisha Sherehe za Miaka 48 ya Mapinduzi ya
Zanzibar huko Bwawani mjini Zanzibar.
Wanafunzi kutoka skuli
mbalimbali ambao walifanikisha Sherehe za Miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar
wakiwa katika karamu maalumu ilioandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza huko Bwawani
Zanzibar
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein wanne kutoka kushoto
akiwa katika picha ya Pamoja na Walimu wa Halaiki ambao walifanikisha sherehe za
Miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar kulia yake ni Makamo wapili wa Rais Balozi
Seif Ali Idi.
No comments:
Post a Comment