Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakicheza ngoma ya
Watemi wa Kisukuma baada kupewa heshima ya kuwa Mtemi Masanja na Mkewe kuwa
Ngole kwenye uwanja wa michezo wa Maswa wakiwa katika ziara ya mkoa wa
Shinyanga Februari 20, 2012. Kushoto ni Mtemi Majebele ambaye ndiye alimpa
heshima hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
RAIA mmoja wa Sweden
aliyefahamika kwa jina la Gunnar ORG Gunnarson (19) amefariki dunia baada ya
gari alilokuwa akisafiria kugongana na gari lingine. Kamanda wa polisi mkoani
hapa, Thobias Andengenye alisema kuwa, tukio hilo limetokea febuari 18 mwaka huu majira ya
saa 7;20 katika barabara ya Arusha-Moshi eneo la Kikatiti wilayani Arumeru
mkoania Arusha. Alisema kuwa, siku tukio gari aina ya Range Rover lenye namba
za usajili T 663 AYB lililokuwa likiendeshwa na Lusingu Lubero Mvungi (38)
mkazi wa jijini Dar es Saalamu likitokea Arusha kuelekea Kia liligongana na
gari aina ya Land Rover Defender lenye namba za usajili T 424 AYD mali
ya Arunga Expedition Arusha Tours. Ambapo gari hilio lilikuwa likiendeshwa na
Francis Paul (45) mkazi wa Sanawari lililokuwa likitoea Moshi kuja Arusha na
kusababisha kifo cha Msweeden huyo ambaye alifariki akiwa anapakiwa kwenye
ndege tayari kwa kwenda Nairobi
kwa matibabu. Andengenye alisema kuwa, ajali hiyo ilitokea baada ya gari aina
ya Range Rover kujaribu kulipita gari liliokuwa mbele yake na kisha kupoteza
uelekeo na kwenda moja kwa moja kugongana na gari aina la Land Rover Defender.
Aidha mbali na ajali hiyo kusababisha kifo hicho,pia ilisababisha majeruhi klwa
kwa watu kumi na moja ambao ni John Halid (60) raia wa Denmark,Bjorn Hoj Glaetesthl
(28)raia wa Denmark, ambao wote kwa pamoja wamepelekwa Nairobi kwa matibabu.
Aidha alitaja majeruhi wengine kuwa ni Francis Paul(45) mkazi wa Sanawari
ambaye amelazwa katika hospitali ya Mount Meru , Clemence Nicolous (32) mkazi
wa Sakina ambaye alitibiwa na kuruhusiwa, Elibariki Nicolous (32) mkazi wa
Sakina ambaye ametibiwa na kuruhusiwa. Aidha wengine ni Godfrey David (21)
mkazi wa Lekulei ambaye ametibiwa na kuruhusiwa, Haruna Amir (31) mkazi wa
Elikulei ambaye alitibiwa na kuruhusiwa, Sajun Mollel (20) mkazi wa Mianzini,
naye alitibiwa na kuruhusiwa , Paulo Omben(34) mkazi wa Sakina ambaye alilazwa
katika hospitali ya Mount Meru. Aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Ombeni
Masawe (26) mkazi wa Mianzini,ambaye amelazwa katika hospitali ya Mount Meru ,na
Lusingu Lubero Mvungi (38) mkazi wa Dar
es salaam ambaye alitibiwa na kuruhusiwa. Aidha
kutokana na tukio hilo ,jeshi nla polisi mkoania
hapa linaendelea kumshikilia dereva wa gari aina ya Range Rover ,Lusingu Lubero
Mvungi (38) mkazi wa jijini Dar es salaam
na kwamba pindi upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili. Wakati huo huo jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu wawili
wajulikanao kwa jina la Linah Christopher( 50)na Elizabeth Christopher(40) wa
maeneo ya ungalimited wakiwa na misokoto 314 ya madawa ya kulevya aina ya bangi
Kamanda alieleza kuwa mafanikio hayo yalitokana na mafanikio ya taarifa
zilizotolewa na raia mwema ambapo mara baada ya taarifa hiyo walikwenda moja
kwa moja katika nyumba ya mtuhumiwa huyo na walipopekua walifanikiwa kupata
bangi hiyo ikiwa imehifadhiwa katika mfuko wa plastiki Hata hivyo watuhumiwa
hao walikiri kuwa walikuwa wamehifadhi bangi hiyo kwa ajili ya kuuza ambapo
jeshi la polisi limeshawafikisha watuhumiwa hao mahakamani ili kujibu tuhuma
ambazo zinawakabili..
No comments:
Post a Comment