NA: GLADNESS MUSHI
TANZANIA inakabaliwa na tatizo la uhaba wa mafundi Sanifu Maabara ambapo kwa sasa wanaozalishwa na Vyuo vya Ufundi hapa nchini hasa Arusha Techical College(ATC)ni ndogo sana hali ambayo inafanya baadhi ya shule za Sekondari hapa nchini kukosa ufanisi zaidi na Masomo ya Sayansi. Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa elimu na Ufundi hapa Nchini Bw Philiph Mulugo wakati akiongea na
wadau mbalimbali wa chuo cha ufundi Arusha(ATC)mapema wiki hii
Aidha Mulugo alisema kuwa bado hali si shwari hasa katika sekta hiyo ya mafundi sanifu wa maabara kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye shule za Sekondari zaidi ya 400 wakati wanaozalishwa wakiwa bado ni 15
Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kuwepo na uhitaji mkubwa sana wa mafundi sanifu kwa kuwa ili shule yoyote ile iweze kufanya vema katika masomo ya Sayansi ni lazima kwanza wataalamu hao waweze kuandaa vifaa mbalimbali vya maabara ili kuruhusu wanafunzi wasome vizuri
Mulugo pia alisema kuwa pamoja na uhaba huo wa mafundi sanifu wa maabara lakini lengo la Serikali la sasa ni kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na Wataalamu hao ambao wataweza kushirikiana na walimu wa Sayansi hivi karibuni ambapo pia hata Vyuo vya ufundi navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekea utaratibu wa kuzalisha wataalamu wengi zaidi
Alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania kuhakikisha kuwa kamwe hawakimbii fani hiyo badala yake wajiunge na Chuo hicho cha Ufundi Arusha ili waweze kudahiliwa kama wataalamu ambapo hali hiyo itaweza kuokoa Jamii ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu hao
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Richard Masika alisema kuwa kwa sasa Jamii inaona Masomo ya Sayansi ni Magumu kwa kuwa hakuna utaratibu wa kuyafundisha kwa vitendo jambo ambalo kwa sasa chuo hicho kimejipanga sana kuweza kujipanga kudahili wahitimu wengi zaidi ili kufanya masomo hayo yasionekane ni magumu
Dkt Masika alisema kuwa ili masomo hayo yasionekane kuwa ni magumu kwa sasa wamejiopanga kwa kuhakikisha kuwa wanazalisha wataalamu wengi zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 watakuwa wamezalisha wataalamu zaidi ya 150 ambao wataweza kusaidia sana kuokoa shule zenye uhaba wa watalaamu hao
No comments:
Post a Comment