Thursday, September 6, 2012

KANISA LA KKKT KILIMANJARO KUWEKEZA KATIKA ELIMU MKOANI KATAVI



Msaidizi wa Askofu Daosisi ya Kaskazini Moshi Mkoani Kilimanjaro wa Kanisa la KKKT Mchungaji Dr Fredrick Shoo pamoja na wadau wengine wa elimu wakiangalia eneo la ujenzi wa shule katika kijiji cha Manga Kata ya Kasokola wilayani Mlele mkoani wa Katavi.

Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kanisa la KKKT Usharika wa Kaskazini Mkoani Kilimanjaro na Arusha watembelea maeneo ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji cha Manga Kata ya Kasokolo wilaya ya Mlele Mkoani Katavi na kueleza nia ya kuvutiwa kuwekezakatika mkoa huo hasa eneo la Manga Kata ya Kasokola.
Wadau hao wa maendeleo walifika ofisi ya Mkurugenzi  Mtendaji wa Wilaya ya Mpanda kuonana na Kaimu Mkurugenzi Mwl.Naomi Nnko ambaye pia ndiye anayekaimu ukurugenzi katika wilaya ya Mpanda na Wilaya ya Mlele alieleza kuwa wawekezaji hao walifika ofisini kwake na kuomba kuja kuwekeza katika sekta ya elimu ambapo Mkurugenzi  huyo alipokea wazo hilo la maendeleo na kulifanyia kazi kisha kuwapeleka wawekezaji kuonana na uongozi wa kijiji cha manga ili kupata Baraka na makubaliano ya kuridhia kutoa eneo litakalotumika kujengaa shule na kuwekeana mikataba.
Kwa upande wake Msaidizi wa Askofu Daosisi ya Kaskazini Moshi Mkoani Kilimanjaro wa Kanisa la KKKT Mchungaji Dr Fredrick Shoo akiwa na Katibu Daiosisi ya Arusha  Ambele Mwaipopo walieleza nia yao kuja kuwekeza katika sekta ya elimu Mkoa wa  Katavi.
Mbali ya wawekezaji hao pia wapo wadau wengine wa maendeleo ambao wanasaidiana na Halmsahauri ya Wilaya ya Mpanda  kwa ajili ya kuwawesha kiuchumi na kielimu kwa kuwawekea miundo mbinu ya maji kwenye shule za msingi na sekondari zilizoko ndani ya makazi ya wakimbizi na shule kadha zile zilizoko nje ya makazi ya wakimbizi.
Mwakilishi wa shirika la kuhudumia wakimbizi Ofisi ndogo ya Mpanda Rose Mchina  alieleza hayo alipotembelea na ujumbe wake ofisini kwa mkurugenzi mtendaji kueleza nia waliyonayo kwa ajili ya kuweka ushirikiano wa maendeleo katika sekta ya  maji na elimu pia

No comments:

Post a Comment