Wanamziki watatu mashuhuri nchini Kenya wameshtakiwa kwa kuchochoea chuki za kikabila kupitia nyimbo zao. Wanamziki hao wanaoimba kwa lugha ya Kikuyu wametoa vibao kumsifia Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta.
Mashtaka hayo yamewasilishwa mahakamani na Tume ya uwiano na Maadili nchini Kenya {NCIC} ambayo iliundwa mwaka wa 2008 kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu.Bw Kinyatta amepinga kuunga mkono wanamziki hao katika kutunga nyimbo za kumsifia.
Watatu hao ni pamoja na Kamande wa Kioi, John De- Mathew, na Muigai Njoroge ambaye ni mwanamziki wa nyimbo za dini na wamekanusha kuchochea chuki za kikabila mbele ya mahakama ya Nairobi.
Uhuru Kenyatta ni mwanawe Mwanzilishi wa taifa la Kenya Jomo Kenyatta na anakabiliwa na kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai-ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi.
Yeye pamoja na Wakenya wengine watatu wamekanusha kuhusika na ghasia hizo ambapo zaidi ya watu 1,300 waliuawa na wengine laki tatu kuachwa bila makao.
Wanamziki hao wameachiwa kwa dhamana.Ikiwa watapatikana na hatia huenda wakafungwa jela miaka mitatu au faini ya dola 12,000.
No comments:
Post a Comment