Saturday, July 21, 2012

SIMBA YA TANZANIA NA VITAL CLUB YA DRC CONGO ZATOKA SARE YA 1-1 U/TAIFA

Mchezaji wa timu ya Simba ya Tanzania Felix Sunzu akimiliki mpira mbele ya Ilongo Ilifo  beki wa timu ya Vital Club  ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo timu hizo zimetoka sare ya magoli 1-1
Kikosi cha timu ya Vital Club kutoka DR Congo kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Simba ya Tanzania kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Simba ya Tanzania wakiwa wamesimama dakika moja kukumbuka waliokufa katika ajali ya boti baharini huko Zanzibar.

No comments:

Post a Comment