Thursday, May 17, 2012

NHC Waazimia Makubwa

Mhandisi na meneja matengenzo wa shirika la nyumba la Taifa-NHC, Julius Ntoga, akisoma maazimio saba yaliyofikiwa na wajumbe
Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Parseko Kone, akifunga mkutano wa baraa kuu la wafanyakazi wa shirika la nyumba la Taifa-NHC,
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la NHC, Nehemia Mchechu, akiongea kabla ya kumkaribisha mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Parseko Kone 
MAAZIMIO YA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI NHC, LILOFANYIKA MJINI SINGIDA.  
1. Tumeazimia kuendelea kutekeleza na kufanikisha malengo yalio katika mpango mkakati wa Shirika wa mwaka 2010 - 2015 katika Kuendelea na ujenzi wa nyumba za makazi na biashara kwa ajili ya kuuza na kupangisha. Malengo hayo ni:
a. Kuwa kiongozi katika uendelezaji miliki
b. Kuwa msimamizi mahiri wa miliki
c. Kuimarisha uwezo wa kiuendeshaji na udhibiti
d. Kutumia rasilimali watu kikamilifu
e. Kupitia upya na kuiboresha mikataba yote na kuboresha mazingira ya kisheria
f. Kuboresha taswira ya Shirika
2. Kwa kutambua ushirikiano mzuri uliopo kati ya Shirika la Nyumba na wadau mbalimbali kama vile Serikali kuu, serikali za mitaa, taasisi za fedha. Tunaahidi kuongeza ushirikiano zaidi na wadau hao ili kuboresha ufanisi na kuondoa vikwazo vinavyozuia na kuchelewesha utekelezaji wa mpango mkakati wetu.
3. Tunaahidi kwamba Shirika litaendelea kuzifanyia matengenezo nyumba zake ili kuziboresha, kuziongezea thamani na muda wa kutumika, na zaidi ya hapo matengenezo hayo yalingane na thamani ya fedha iliyotumika. Hii inaboresha taswira ya Shirika na huduma bora kwa wateja.
4. Pamoja na kujenga nyumba za gharama ya kati na juu, tumejipanga kujenga nyumba za bei nafuu katika wilaya mbalimbali nchini. Ili kuwawezesha watu wenye kipato cha chini kumiliki nyumba na kujiona kuwa taifa lao linawathamini kupitia shirika la Nyumba la Taifa.
5. Kuendelea kuwa karibu na jamii kwa kuhakikisha kwamba Shirika linatoa huduma kwa jamii mbalimbali hapa nchini ili kujenga mahusiano mazuri na kuongeza ajira kwa vijana na jamii kiujumla.
6. Kwa pamoja tunaazimia kufanya kazi kwa bidii, ufanisi, nidhamu, uadilifu, uaminifu, na kuzingatia maadili yetu ya msingi na kuhakikisha kwamba tunafikia malengo yetu tulio jiwekea.
7. Kuendelea kufanyia marekebisho ya kodi ya pango ili iendane na soko na kuongeza pato la shirika ili liweze kujenga nyumba nyingi zaidi.

No comments:

Post a Comment