Wednesday, March 21, 2012

Rais Azindua Mradi Wa Maji Pawaga

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI PAWAGA ASIFU MCHANGO WA TAASISI ZA DINI NCHINI ...
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa serikali yake itaendelea kuchangia mradi wa maji wa kata ya Pawaga jimbo la Isimani Wilaya ya Iringa vijijini uliojengwa na Kanisa la Aglicana dayosisi ya Ruaha kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.
Amtaka mhandisi wa maji mkoa wa Iringa Amosi Byemelwa kufika katika kata ya Pawaga baada ya wiki moja ili kushughulikia tatizo la mfereji wa Mlenge ambao ni kero kubwa katika kilimo cha mpunga.
Rais Kikwete ataka wananchi kufikisha taarifa ya kutofika kwa meneja huyo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christina Ishengoma ili afikishe taarifa kwake juu ya utekelezaji wa ahadi hiyo.
Akiwahutubia wananchi wa Pawaga jimbo la Isimani Jana baada ya kuzindua mradi huo mkubwa wa maji ,Rais Kikwete alisema kuwa serikali yake inatambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi Za dini na kupongeza .
Rais Kikwete alisema kuwa serikali imejipanga katika kuboresha Huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo huduma ya maji hivyo kuwataka wananchi kuendelea kujenga imani na serikali Yao.
Katika mkutano huo Rais Kikwete akitumia muda wa zaidi ya dakika 20 kusikiliza kero za wananchi kupitia madiwani wa kata tatu za eneo hilo kabla ya kuanza kutolea majibu ya matatizo ya wananchi.
Aidha Rais Kikwete alihoji Sababu ya wananchi wa kata ya mlenge kuendelea kukosa Huduma ya afya huku vituo vya Pawaga kukosa dawa wakati serikali ikiendelea kutoa fedha kwa ajili ya dawa .
Kabla ya kufika katika mkutano huo na wananchi Msafara wa Rais Kikwete ulizuiwa na wananchi wa kijiji cha Kinyika ambao wlikusanyika kando kando ya barabara ili kutaka kufikisha kilio chao cha uhaba walimu katika shule ya sekondari Wiliam Lukuvi.
Kuhusu kero ya barabara Rais Kikwete aliagiza wilaya ya Iringa na mkoa kuendelea kuboresha barabara ili kukuza uchumi wa wakulima wa maeneo hayo.
Huku alisema kuwa suala la uhaba wa walimu serikali unaendelea kuongeza walimu kwa kuajiliwa walimu 25000 na kuwa itaendelea kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment