Thursday, March 22, 2012

Milioni Mia Tatu Kusaidia Huduma Ya Maji Iringa



Na Mwandishi Wetu

 ZAIDI YA SHILINGI Milioni 300 zimetolewa ili kuboresha huduma ya maji

katika mkoa wa Iringa, na katika Hospitali ya Manispaa ya Iringa.

Akizungumzia mpango huo mbele ya naibu waziri wa maji Gerson Lwenge,
ofisa mahusiano wa kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Tedy Mapunda,
amesema kampuni imemeamua kuwekeza katika huduma ya maji kwa jamii.

Tedy amesema kati ya fedha hizo, shilingi milioni 200 mwaka huu
wamewekeza katika miradi salama ya maji, ikiwa pamoja na uvunaji wa
maji ya mvua katika Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa.

Amesema wameanzisha mpango wa kutoa elimu kwa jamii, ili kuvilinda
vyanzo vya maji na miundombinu yake, ikiwa pamoja na kuweka matenki ya
lita elfu 60 kwa ajili ya kuvuna maji katika Hospitali hiyo.

Aidha amesema lengo la mpango huo ni kurejesha huduma kwa jamii,
kutokana na kampuni hiyo ya Serengeti kutumia huduma ya maji kwa
kiwango kikubwa katika uzalishaji wa bidhaa zake.

Naye Naibu waziri Lwenge amezindua ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji
ya mvua, ambalo litagharimu zaidi ya shilingi Milioni 50 zinazotolewa
na Kampuni ya Serengeti, huku Milioni 150 zitapelekwa katika Hospitali
ya Seketule Mwanza pamoja na Hospitali ya Mawenzi Kilimanjaro na Dar
es salaam katika Hospitalia ya Temeke.

Siku ya maji kitaifa inafanyika katika mkoa wa Iringa, ambapo mgeni
rasmi ni rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, jakaya Kikwete,
ambaye tayari amezindua miradi kadhaa ya maji mkoani hapa, ukiwemo wa
mradi wa umwagiliaji wa Pawaga

No comments:

Post a Comment