Kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Jimbo la singida mashariki inayomkabili Mbunge wa Bunge wa Jimbo hilo jana ilikuwa kivutio, baada ya Chama cha Mapinduzi ambao ni walalamikaji kumwomba wakala wa CHADEMA kutoa ushahidi.
Wakala huyo, Mghenyi Hasani Kimu, alifika mahakamani, na kudai kuwa hakua anajua kuwa ameitwa mahakamani kufanya nini. Huku akiulizwa maswali na alimgeuka wakili wake na katika maelezo ikabainika kuwa tuhuma za Tundu Lisu zilikuwa uzushi tu; Baada ya shahidi kuwageuka CCM mahakamani walitaka kumgeuka shahidi waliyemleta kuwa wamempa rushwa, lakini jaj alikataa kwa kuwa suala hilo halikuwa katika mashtaka:
Baadhi ya mahojiano yalikuwa hivi:
Maswali yaliulizwa na wakili wa kujitegemea Gabriel Wasonga, anayewatetea walalamikaji
Unakaa wapi?
Kijiji cha Isuna B. Kata ya Issuna.
Unajua umeitwa wapi hapa?
Mahakamani.
Unajua umeitwa kwa ajili ya nini?
SIFAHAMU.
Mimi nimeletewa Samansi mahakamani, nimeambiwa kuja mahakamani, hivyo nimekuja nielezwe kuna nini hapa mahakamani.
Unakumbuka umeshiriki uchaguzi siku za hivi karibuni?
Uchaguzi upi, mdogo au mkubwa.
Uchaguzi Mkuu:
Mimi nilishiriki, kama mpiga kura, ila pia nilikuwa wakala,
Matokeo yalikuwa na shida gani katika kituo chako?
Hakukuwepo na tatizo, matokeo yalikuwa halali kabisa, mbele ya Mungu
Ili mtu aseme kuwa mimi ni mpiga kura unapaswa kuwa na nini?
Shahada ya kupiga kura
Umesema kuwa ulishiriki kama mpiga kura, je ulipiga kura wapi?
Kituo cha Issuna Shule ya msingi namba 2.
Nini ambacho ulikitumia kupigia kura?
Sijakuelewa, rudia.
Nini ambacho ulitumia kuonyesha ili upige kura?
Nilionyesha kadi ya mpiga kura, na hati ya kiapo kwa kuwa nilipiga kura katika eneo ambalo sikuandikishwa.
Ulishiriki kama wakala wa Chama gani?
CHADEMA.
Wewe ulikuwa kituo gani?
Kituo cha Shule ya msingi Isuna, kituo namba mbili.
Mawakala mlikuwa wangapi?
Nadhani walikuwa kama wane hivi
Unaweza kukumbuka Vyama vilivyoshiriki uchaguzi?
Nakumbuka baadhi
Tutajie.
CCM, CHADEMA, TLP, APPT MAENDELEO, CUF, vingine sikumbuki.
Wagombea walikuwa wangapi?
Wagombea wa nafasi gani?
Wewe ulisimamia uchaguzi wa wagombea gani?
Udiwani, Ubunge, na Urais.
Katika Kituo hicho wakala wa CHADEMA Alikuwa nani?
Nilikuwa mimi.
Je wa CCM alikuwa nani?
Robert Mtua Kimani.
Wa CUF alikuwa nani?
Jumanne maulidi.
APPT Maendeleo alikuwa nani?
Magreti Hasani.
Ieleze Mahakama, kabla ya kwenda kuwa wakala, ulipata mafunzo yeyote?
Ndiyo.
Wapi?
Shule ya Msingi Minang’ana, awamu yakwanza, na y a pili nimepatia shule ya sekondari Issuna
Katika wote mliofundishwa, mlikuwa wanachama wa chama gani?
Mafundisho yalikuwa ni ya wanachama wa CHADEMA
Una maana wote mliopewa mafunzo ndo mlienda kusimamia kura?
NDIYO.
Hebu tusaidie, nani aliwagawia vituo?
Tulienda kuapa kwenye mahakama ya Ikungi, ndo tukapewa hati ya kiapo na kupangiwa vituo.
Katika kusimamia kazi hiyo kama wakala mlilipwa?
Hakuna malipo yeyote, isipokuwa maji, chakula na soda.
Hayo mliambiwa wapi?
Tuliambiwa baada ya kuapa, tulipopangiwa kazi.
Mafunzo yalitolewa na nani?
Tundu Lissu.
MAHOJIANO NA MLALAMIKIWA, WAKILI MWENYE KESI-TUNDU LISSU:
T/L: shahidi, ntakuuliza maswali naomba ujibu kusaidia mahakama. Sawa?
T/Lnitakuwa nimekosea nikisema wewe ni mkaazi wa Isuna B?
P/W: UTAKUWA HUJAKOSEA.
Nitakuwa nimekosea nikisema kwamba Mwenyekiti wa kijiji chako anatoka CCM
P/W/ hujakosea
Nitakuwa nimekosea kukuambia kuwa huyu ndiye mwenyekiti aliyekufuata uje Mahakamani kukuomba uje Mahakamani kutoa ushahidi?
PW.hujakosea, yeye ndiye aliyenileta hapa.
Je nitakuwa nimekosea, nikisema kuwa baada ya kukueleza haya, ulienda naye nyumbani kwa Jonathani Njau?
UTAKUWA UMEKOSEA.
Uliwahi kwenda kwa Njau siku za hivi karibuni?
SHAHIDI: Sijaenda.
Umewahi kuonana na Marcel Hallu, aliyenishtaki?
Sijawahi kumwona, simjui ni wa wapi?
Mkti wa Kijiji alipokuja kukuambia unahitajika Mahakamani, alikuambia unakuja kutoa ushahidi gani?
SHAHIDI: Nilimuuliza Mahakama ipi? Aliniambia wewe ulikuwa wakala? Nikamjibu ndiyo.
Mwenyekiti akaniambia kuwa uende ukaeleze uchaguzi livyokuwa.
SHAHIDI: Nilimuuliza Nani anashtakiwa?
SHAHIDI:Mwenyekiti akaniambia utajua huko huko mahakamani.
T/L. Ieleze mahakama, nani amekulipia nauli ya kuja hapa kwa ajili ya kuja kutoa ushahidi?
SHAHIDI: Mwenyekiti wa Kijiji ndiye alilipa kila gharama.
T/L. Ninavyofahamu mimi wakristu wanatumia amri kumi za Mungu na Moja inakataza kusema uongo, mweleze jaji, je umepewa shilingi ngapi kuwa shahidi?
Alinilipia, Nauli Chakula, na Nyumba ya Kulala. Nimelala super Kitasa Guest.
Kwa vile hukuwa na pesa, unaweza kumwambia jaji, nani alikulipia guest?
Mwenyekiti alilipa yeye.
Asubuhi ya leo umekunywa chai, na mchana ukapata chakula cha mchana kabla hujaja hapa?
Ni mwenyekiti wa Kijiji cha Isuna ndiye aliyenilipia.
Mweleze Jaji, ukweli kulingana na mafundisho ya dini yako. Uliwahi kwenda kwa Njau?
Sijawahi kwenda, mbona unanifuatiliafuatilia?
T/L. Umeeleza mahakama kuwa ulikuwa wakala wangu, kituo cha Isuna, unavyomfahamu yeye ni mwanachama wa Chama gani?
Sijui ni wa CHAMA gani. Ila najua kuwa alihudhuria mafunzo ila hakuwa na nafasi ya uwakala.
T/L. Kwa vile mlikuja kuhudhiria mafunzo ya uwakala niliyotoa, hivyo wathibitisha kuwa walikuwepo na wa CCM, CUF, na vyama vingine sio CHADEMA tu?
NDIYO:
Ulipokuwepo ndani ya kituo uliona mawakala waliokuwepo nje?
Nisingeweza maana hawakuwa na sare,
T/L: Je ni makosa kwa mgombea kuwalisha mawakala wake?
Kama makosa basi mtakuwa mlikosea wote, maana wote waliletewa chakula.
T/L. Maji. Soda na Biskuti uliletewa na nani?
SHAHIDI: Nililetewa na Gineton bulali mgombea wa udiwani katika kata yangu
T/L. Nitakuwa nimekosea kusema kuwa yeye ndo alipaswa kukuletea chakula Isuna, maana yeye alikuwa Mgombea?
Hujakosea. Maana wote walikuja wakaingia.
T/L Kwa vile wewe ulikuwa wakala wa ndani, unafikiri ilikuwa ni kosa kukuletea maji, soda na biskuti?
SHAHIDI; Hajakosea.
T/L. Katika kesi iliyofunguliwa hapa nimeambiwa niliwapa rushwa je ni kweli?
SHAHIDI; Hiyo haikuwa rushwa, maana ingalikuwa rushwa ingalitolewa pembeni sio hadharani.
T/L; ulienda na usafiri gani/
Shahidi: Kwa miguu yangu
T/L; hii tuhuma ya kuhonga wewe shahidi uanionaje?
SHahidi: Siwezi kujua
T/L: Hizi tuhuma za kuhonga mawakala ninazushiwa?
Shahidi; ni uzushi tu. Wewe unazushiwa
Katika Kituo chako, nani alishinda?
Wagombea wote wa CCM, yaani Diwani CCM, Mbunge CCM, na rais wa CCM.
Walionishtaki wameomba mahakama ifute matokeo ya uchaguzi huo ambao wewe ulikuwa wakala;
SHAHIDI; Sioni sababu yakufuta matokeo, matokeo yalikuwa halali.
Wakili wa serikali:
Je ulipokuwepo mahakamani kulikuwa na tatizo lolote?
SHAHIDI: Hakukuwa na shida., mimi sikuona tatizo lolote.
Je kuna wakala aliyejaza fomu ya malalamiko kituoni kwako?
Ndiyo, wakala wa ccm.
Alilalamikia nini?
SHAHIDI: Mara ya kwanza jamaa wa CCM alilalamika, lakini baadaye alipoona kuwa wagombea wake wameishinda alichana fomu ya malalamiko.
JAJI: Uliposimamia ulikuwa Chama gani?
Shahidi: Mimi nilikuwa CHADEMA
JE SASA HIVI WEWE NI CHAMA GANI?
NIPO CHADEMA.
JAJI: aje shahidi mwingine
Wakili: mheshimiwa Jaji, shahidi wangu ameondoka simwoni alipokwenda.
JAJI ameahirisha kesi itaendelea kesho (leo)
No comments:
Post a Comment